Pata taarifa kuu
BURUNDI-UPINZANI-CENI-UTAWALA-SIASA-USALAMA

Céni  yakutana na wanasiasa Burundi

Mkutano kati ya tume huru ya uchaguzi (Céni), serikali ya Burundi, vyama vya siasa pamoja na wawakilishi wa vyama vya kiraia wamekutana Jumatatu Desemba 22 ili kutathimini matokeo ya zoezi la kuandika wapiga kura liliyotamatika wiki mbili zilizopita.

Mwenyekiti wa tume huru ya uchaguzi nchini Burundi (Céni), Pierre Claver Ndayicariye.
Mwenyekiti wa tume huru ya uchaguzi nchini Burundi (Céni), Pierre Claver Ndayicariye. DR.
Matangazo ya kibiashara

Mkutano huo umefanyika wakati ambapo kunashuhudia mvutano kati ya upinzani na tume huru ya uchaguzi (Céni) kuhusu matokeo ya zoezi hilo.

Jumamosi Desemba 20 vyama 9 vya upinzani viliomba mkutano huo usiongozwe na tume huru ya uchaguzi, bali kitafutwe chombo kingine ambacho kitaweza kusimamia mkutano huo, hususan  Baraza la viongozi wa dini.

Hivi karibuni vyama 18 vya upinzani viliomba tume huru ya uchaguzi ifute matokeo ya uchaguzi na zoezi hilo liliyotamatika wiki mbili zilizopita, lirejelewe upya bila masharti, la sivyo tume hiyo ijiuzulu.

Vyama vya kiraia zaidi ya 200 katika mkutano na vyombo vya habari, viliomba hivi karibuni tume huru ya uchaguzi ifute matokeo ya zoezi la wapiga kura, vikibani kwamba zoezi hilo liligubikwa na kasoro nyingi.

Ijumaa Desemba 19 katika mkutano na vyombo vya habari na raia, rais wa Burundi, Pierre Nkurunziza, amesema hakuna ibara katika sheria ya uchaguzi inayoeleza kufutwa kwa matokeo ya uchaguzi, na kuwaonya wanasiasa kutoendelea na kuifanyia vitisho tume huru ya uchaguzi au kuiingilia katika kazi yake.

Hata hivyo, vyama 18 vya upinzani vilitishia hivi karibuni kuwahimiza wafuasi wao kuingia barabarani iwapo madai yao hayatopatiwa ufumbuzi.

Itakumbuka kwamba siku chache baada ya zoezi la kuandika wapiga kura kuanza upinzani, vyama vya kiraia pamoja na Kanisa Katoliki viliomba tume huru ya uchaguzi ifute zoezi hilo kufuatia baadhi ya dosari kujitokeza, hususan vitambulisho vya uraia bandia ambavyo vilikua vikitumiwa kwa kujiorodhesha katika zoezi hilo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.