Pata taarifa kuu
KENYA-UPINZANI-Siasa-Usalama

Kenya : upinzani waandaa mkutano kabambe

Nchini Kenya, muungano wa upinzani CORD unaanda mkutano wake wa kisiasa jumatatu wki hii leo katika bustan ya Uhuru Park jijini Nairobi, siku ya Sabasaba siku ambayo mwaka 1990 upinzani uliandamana dhidi ya serikali ya wakati huo ukushinikiza kuwepo kwa vyama vingi.

Muungano wa upinzani nchini Kenya (CORD) unandaa mkutano kabambe.
Muungano wa upinzani nchini Kenya (CORD) unandaa mkutano kabambe. (Photo : Reuters)
Matangazo ya kibiashara

Kiongozi wa muungano wa upinzani nchini Kenya (CORD), Raila Odinga.
Kiongozi wa muungano wa upinzani nchini Kenya (CORD), Raila Odinga. Photo : Khaled Desouki /AFP

Muungano wa CORD unaongozwa na aliyekuwa Waziri Mkuu Raila Odinga unafanya mkutano huu , kwa kile vigogo wa muungano huo wanasema watazungumza na wakenya baada ya serikali kukataa wito wao wa kuzungumza nao kuhusu maswala mbalimbali yanayotokea ncnini humo.

Hata hivo polisi imetahadharisha kufanyika kwa mkutano huo iwapo itapata taarifa ya kuhatarishwa kwa usalama. Mkuu wa polisi nchini Kenya, David Kimayo, amesema iwapo kutatokea vurugu na kusababisha hasara, wahusika watafikishwa mbele ya vyombo vya sheria. Serikali kwa upande wake imesema hapingi mkutano huo unaoandaliwa na CORD.

Askari polisi katika mji wa Nairobi nchini Kenya.
Askari polisi katika mji wa Nairobi nchini Kenya. REUTERS/Noor Khamis

“Sisi tunaheshinu katiba, nakatiba ndio inawaruhusu kufanya mkutano wao, lakini kwa amani na utulivu”, amesema naibu rais wa Kenya, william Ruto.

Balozi Bethwel Kiplagati, aliekua mwenyekiti wa tume ya ukweli, haki na maridhiano nchini Kenya amependekeza kuwepo na mazungumzo ya kitaifa katika hali ya kulijenga taifa.

Hayo yakijiri, Polisi Pwani ya Kenya wanawasaka watu wanaominiwa kuwa wafausi wa vuguvugu la MRC wanaotuhumiwa kutekeleza mauaji ya zaidi ya watu 20 katika Kaunti ya Lamu mwishoni mwa juma lililopita.

Mauaji hayo yalitokea katika miji ya Hindi na Gamba, na yamekuja wiki kadhaa baada ya mauaji mengine kama hayo kutokea katika Kaunti hiyo na kusababisho zaidi ya watu 60 kupoteza maisha.

Kundi la kigaidi la Al Shabab kutoka nchini Somalia lilikiri kutekeleza shambulizi hilo kwa sababu ya jeshi la Kenya kuwa Somalia lakini, polisi nchini Kenya inasema si kweli kwa kile wanachokieleza mauaji hayo yalitekelezwa na kundi la MRC.

Naibu rais wa Kenya, William Ruto.
Naibu rais wa Kenya, William Ruto. REUTERS/Noor Khamis

Naibu wa rais wa Kenya William Ruto amewapa polisi saa 48 kuwasaka na kuwakamata wauaji hao.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.