Pata taarifa kuu
SOMALIA

Kundi la Al Shabab laelezwa kuwa na uwezo wa kutekeleza mashambulizi zaidi nje ya mipaka ya Somalia

Mwakilishi maalum wa Umoja wa Mataifa nchini Somalia Nick Kay,ameonya kuwa wanamgambo wa kundi la kigaidi la al Shabab wana uwezo na dhamira ya kueneza mashambulizi yao nje ya ngome zao nchini Somalia,na kutoa wito kwa nchi za ukanda wa Afrika mashariki kushirikiana zaidi kupambana na tishio hilo.Β 

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki Moon akiwa jijini Nairobi Kenya 28 Juni 2014
Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki Moon akiwa jijini Nairobi Kenya 28 Juni 2014 nation.co.ke/JEFF ANGOTE
Matangazo ya kibiashara

Kay amesema kuwa kundi la Al Shebab ni shirika ambalo lina agenda ya kikanda," alisema Nick Kay, maalum wa Umoja wa mwakilishi katika Somalia na kwamba uongozi wa juu wa shirika hilo unajiona ukitafuta kufanya jambo fulani nje ya taifa la Somalia.

Hapo jana katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki Moon amesema kuwaΒ  umoja huo uko tayari kuisaidia nchi ya Kenya na mataifa mengine barani Afrika kupambana na ugaidi , kufuatia mfululizo wa mashambulizi yaliyosababisha vifo nchini Kenya.

Akizungumza akiwa jijini Nairobi BanΒ  amesema amezungumza na rais wa Kenya Uhuru Kenyatta kwa urefu kuhusu namna ambavyo Umoja wa Mataifa na serikali ya Kenya zitafanya kazi kwa pamoja kushughulikia mashambulizi hayo ya kikatili.

Kundi la Al Shabab hivi karibuni limeongeza mashambulizi dhidi ya nchi zinazochangia kikosi imara cha wanajeshi elfu 22,000 wa Umoja wa Afrika wanaoungwa mkono na Umoja wa Mataifa,waliopelekwa nchini Somalia kupambana na kundi hilo tangu mwaka 2007.
Β 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.