Pata taarifa kuu
JAMHURI YA KIDEMOKRASIA YA CONGO

Kiongozi wa Upinzani nchini DRC alazwa Hospitalini

Mwenyekiti wa Chama cha Upinzani cha Demokrasia na Maendeleo ya Ustawi wa Jamii- UDPS- nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo bw. Etienne Tshisekedi anasadikiwa kulazwa hospitalini tangu siku nyingi, madai ambayo yanatupiliwa mbali na familia yake.

Matangazo ya kibiashara

Likizungumzia kutoweka kwenye ulingo wa kisiasa kwa mpinzani huyo, jarida la habari la Ufaransa la Jeune Afrique linahakikisha kwamba Tshisekedi ambaye sasa anatimiza umri wa miaka 82 anasumbuliwa na kiharusi na kuwa amelazwa katika hospitali ya Monkole Mont Ngafula tangu tarehe 20 mwezi Mei mwaka huu.

Vyanzo vinavyoaminika vimezungumzia mkanganyiko uliopo katika kubaini Etienne Tshisekedi yuko wapi na anashugulika na nini wakati ambapo inasemekana kuwa familia yake na hasa mke wake wamepunguza idadi ya watu wanaomtembelea mpinzani huyo na kuwa huenda hata miguu yake imedhoofika.

Familia ya bwana Tshisekedi kwa upande wake inahakikisha kuwa mpinzani huyo bado anadunda huku akijisomea, akichapa kazi na kutoa maelekezo na maagizo kwa makada wa chama chake na kuwa habari hizo ni tetesi zisizo na msingi.

Etienne Tshisekedi hajaonekana mbele ya watu wengi tangu mwezi Februari, huku kukiwa na hali ya sintofahamu kwenye chama chake kuhusu mtu ambaye anatakiwa kuchukuwa nafasi yake hasa baada ya kumfuta kazi mkurugenzi wa ofisi yake Albert Moleka wiki kadhaa zilizopita kwa taarifa iliyosainiwa na Katibu Mkuu wa chama cha UDPS.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.