Pata taarifa kuu
DRCONGO-MAPIGANO

Makabiliano yazuka upya kaskazini mwa Goma kati ya waasi wa M23 na jeshi la FRDC

Siku chache baada ya mazungumzo ya amani kukwama makabiliano yameendelea ijumaa kati ya makundi ya waasi wa M23 dhidi ya jeshi nchini jamuhuri ya demokrasia ya Congo,pande zote mbili zimethibitisha sambamba na Umoja wa Mataifa.

Makabiliano yaibuka tena kaskazini mwa Goma kati ya waasi wa M23 na jeshi la FRDC
Makabiliano yaibuka tena kaskazini mwa Goma kati ya waasi wa M23 na jeshi la FRDC un.org
Matangazo ya kibiashara

Makabiliano yameripotiwa kutokea eneo la kilomita 25 kaskazini mwa mashariki ya jiji la Goma,kwa mujibu wa msemaji wa waasi Vianney Kazarama.

Pande mbili zimetuhumiana kuanzisha mashambulizi ambapo Kazarama amesema jeshi la Congo DR lilianza mashambulizi alfajiri.

Hata hivyo msemaji wa upande wa jeshi la serikali Olivier Hamuli,jimboni Kivu, alisema waasi walishambulia jeshi la Congo na kusababisha makabiliano.

Chanzo kimoja kutoka kwa waangalizi wa amani wa Umoja wa Mataifa MONUSCO,kimeeleza waasi walianzisha mashambulizi.

Chanzo kimoja kiliomba kutotajwa jina kilibainisha kuwa Mapambano yanaendelea na mpaka sasa bado haijajulikana kama kuna watu waiojeruhiwa au la.

Mapema jumatatu pande zote mbili zilithibiotisha kuahirisha mazungumzo ya amani yaliyokuwa yakifanyika jijini Kampala nchini Uganda pamoja na jitihada za Umoja wa Mataifa kuhimiza juhudi za kukomesha mapigano huko mashariki mwa DRCongo.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.