Pata taarifa kuu
CONGO-DRC

DRC na Congo-Brazzaville zatunishiana misuli kuhusu kurejeshwa nyumbani kwa raia wake

Mazunguzo kati ya Serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo DRC na ujumbe maalumu wa Serikali ya Congo-Brazzaville hii leo yanaingia kwenye siku yake ya pili mjini Kinshasa, mazungumzo yanayolenga kuondoa tofauti zilizojitokeza hivi karibuni baada ya utawala wa Congo-Brazzaville kuwarejesha nyumbani maelfu ya rais wa DRC. 

Rais wa DRC, Josephu Kabila (kushoto) akisalimiana na rais wa Congo-Brazzaville, Dennis Sassou Nguesso
Rais wa DRC, Josephu Kabila (kushoto) akisalimiana na rais wa Congo-Brazzaville, Dennis Sassou Nguesso DRCgvt
Matangazo ya kibiashara

Katika kipindi cha miezi miwili iliyopita, takriban watu laki moja na elfu arobaini wamelazimika kuvuka mpaka baada ya kufukuzwa katika mazingira tatanishi na kuzua mgogoro wa kidiplomasia baina ya nchi hizo jirani.

Le président Kabila en septembre 2013 au sommet de Kampala.
Le président Kabila en septembre 2013 au sommet de Kampala. Reuters

Hali hii ya kufurushwa kwa raia wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo nchini Congo-Brazzaville ilitishia kuvunjika kwa uhusiano wa muda mrefu uliokuwepo baina ya nchi hizi mbili kutokana na mwingiliano wa raia wake.

Juma hili pia rais Josephu Kabila alilazimika kuzungumzia hatua ya Congo-Brazzaville kuwarudisha nyumbani raia wake na kutaka kufanyika kwa mazungumzo ili kufahamu undani wa hatua ya taifa hilo kuwamua kuwarudisha kwa nguvu raia wake.

Kufuatia kurejea nchini mwao na hata baadhi yao kukosa mahali pakuishi kutokana na maisha yao yote kuwa nchini Congo-Brazzaville, ilisababisha pia hata raia wa Congo nao kuanza kurejea nchini mwao kwa hiari kuhofia vurugu zinazoweza kujitokeza.

Rais wa Congo-Brazzaville, Denis Sassou Nguesso
Rais wa Congo-Brazzaville, Denis Sassou Nguesso REUTERS/Tiksa Negeri

Waziri wa mambo ya ndani wa DRC na kiongozi wa ujumbe wa nchi hiyo katika majadilianao hayo Richard Muyej amekosoa na kushutumu operesheni hiyo aliyoiita kuwa ya kikatili pamoja na ukiukwaji wa haki za binadamu.

Madai haya ya Serikali ya DRC na Umoja wa Mataifa kuhusu kuwepo kwa vitendo vya ukiukwaji wa haki za binadamu unaofanywa na maofisa wanaotekeleza operesheni hii, yalikanushwa vikali na tawala wa Congo-Brazzaville.
.
Kwa upande wa Congo-Brazaville, msimamo wao ulionekana kutoyumbishwa na shutma hizo, huku wakiahidi kuendelea na operesheni hiyo kwa kuzingatia taratibu za kisheria, kama alivyoeleza waziri wa mambo ya ndani wa Congo-Brazzaville, Raymond Mboulou.

Naye Gavana wa Jimbo la Kivu Kaskazini Julien Paluku aliyehitimisha ziara yake katika makambi walioko raia hao wa DRC waliorejeshwa mjini Kinshasa amesema kuwa operesheni hiyo ilikiuka haki za bianadamu na haikubaliki.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.