Pata taarifa kuu
JAMHURI YA AFRIKA YA KATI

Wanajeshi wa Congo Brazzaville, Cameroon, Gabon na Chad kuwadhibiti Waasi wa Seleka kufika Bangui

Matarajio ya Waasi wa Seleka kuuweka kwenye himaya yao Mji wa Bangui nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati yameanza kutoweka kufuatia nchi jirani kupeleka wanajeshi wake kuisaidia serikali ya Rais Francois Bozize aliyekataliwa msaada wa kijeshi kutoka kwa Ufaransa na Marekani.

Kundi la Waasi la Seleka linalopambana kuudhibiti Mji wa Bangui huenda likakabiliwa na upinzani kutoka kwa majeshi ya nje
Kundi la Waasi la Seleka linalopambana kuudhibiti Mji wa Bangui huenda likakabiliwa na upinzani kutoka kwa majeshi ya nje
Matangazo ya kibiashara

Serikali ya Rais Bozize imeanza kupata ahueni baada ya Gabon, Congo Brazzaville na Cameroon kutuma wanajeshi mia moja ishirini kusaidiana na wengine mia nne wa Chad ili kukabiliana vilivyo na Waasi wa Seleka ambao wameendelea kuwa kitisho kwa usalama baada ya kuchukua Miji mingine kadhaa.

Wanajeshi hao wamekwenda Bangui chini ya Mwamvuli wa Kikosi cha Afrika cha Kulinda Amani FOMAC na watakuwa na jukumu la kuhakikisha wanaulinda Mji wa Damara ambao ni muhimu kwa sasa kabla ya Waasi wa Seleka kufika Bangui.

Mji wa Damara unaonekana ndiyo sehemu muhimu kimkakati baina ya Waasi wa Seleka na Kikosi cha Serikali na kunatarajiwa kutokea mapigano makali baina yao kipindi hiki ambacho Waasi wakiwa wamebakiza kilimoeta mia moja sitini kufika Bangui.

Ujio wa wanajeshi hao unajiri kipindi hiki ambacho machafuko yangali yakiendelea kushuhudiwa katika Jiji la Bangui kati ya wafausi wanaosemekana wa Seleka na Wanajeshi wa Serikali baada ya kuuawa kwa kijana mmoja wa kiislam.

Kifo cha kijana huyo wa Kiislama ambaye anahusishwa na Waasi wa Seleka kumechangia vurugu ambazo zimesababisha kifo cha askari mmoja na hivyo kuzusha hofu huenda kukaanza kutokea machafuko ya kidini.

Mataifa ya Afrika ya Kati yameonekana kuchukuziwa na hatua ya Waasi wa Seleka kusonga mbele pasi na kukutana na upinzani hivyo wameweka mkakati mahsusi kuhakikisha wanaisaidia vilivyo serikali ya rais Bozize iliyozidiwa nguvu.

Msemaji wa Waasi wa Seleka Eric Massi alinukuliwa juzi akikataa kuketi mezani na serikali ya Rais Bozize na badala yake walikuwa wanashinikiza kuondoka madarakani kwa Kiongozi huyo.

Ufaransa yenyewe ilipeleka wanajeshi wake mia moja ishirini Jijini Bangui kwa ajili ya kulinda wananchi wake pamoja na maslahi yao na si kuisaidia serikali ya Rais Bozize ambaye aliomba msaada.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.