Pata taarifa kuu
SUDANI KUSINI-Mazungumzo

 Salva Kiir na Riek Machar uso kwa uso

Rais wa Sudan Kusini, Salva Kiir hii leo anatarajiwa kukutana ana kwa ana na aliyekuwa makamu wake wa rais na sasa ni kiongozi wa waasi wa nchi hiyo, Riek Machar, mkutano unaokuja kwa viongozi hawa kujaribu kumaliza tofauti zao na kuleta amani nchini humo.

Rais wa Sudani Kusini, Salava Kiir (kushoto), akiwa pamoja na rmakamu wa zamani wa rais, Riek Machar (kulia).
Rais wa Sudani Kusini, Salava Kiir (kushoto), akiwa pamoja na rmakamu wa zamani wa rais, Riek Machar (kulia). REUTERS/Goran Tomasevic/Files
Matangazo ya kibiashara

Rais wa Sudani Kusini, Salva Kiir ameondoka Juba leo akielekea Addis Ababa, mji mkuu wa Ethiopia, ambako atakutana na makamu wake wa zamani Riek Machar, ambaye kwa sasa ni hasimu wake. Ni kwa mara ya kwanza vigogo hao wawili wanakutana tangu yalipoanza machafuko desemba 15 mwaka 2013.

Taarifa za hivi punde zinaeleza kuwa tayari kiongozi wa waasi Dr Riek Machar amewasili mjini Juba usiku wa jana na kwamba rais Salva Kiir anatarajiwa kuwasili muda mfupi ujao mjini Addis tayari kwa mazungumzo yanayolenga kumaliza mapigano kwenye nchi yao.

Hailemariam Desalegn, pamoja na ujumbe wa mamlaka ya mataifa ya mashariki (Igad) ambao unasimamia mazungumzo kati ya pande zinazokinzana.

Makamo wa zamani wa rais wa Sudani Kusini, Riek Machar.
Makamo wa zamani wa rais wa Sudani Kusini, Riek Machar. REUTERS/Goran Tomasevic

"Ujumbe huo unatazamiwa kuandaa agenda ya mazungumzo, lakini sidhani kwamba Riek Machar atakuana leo ana kwa ana na Salva Kiir. Sio leo kwa kweli”, amesema mmoja kati ya wasemaji wa Riek Machar, Peter Gadet Dak.

Riek Machar, ambaye alitimuliwa madarakani na Salva Kiir kutokana na malumbano kati yao kuhusu uongozi wa chama madarakani, aliamua kuanzisha vita vya maguguni dhidi ya utawala wa Salva Kiir, baada ya kutuhumiwa kupanga njama za kupindua utawala wake.

Tuhuma hizo dhidi ya Machar zilitolewa na mkuu wa majeshi ya Sudani Kusini, wakati mapigano yalipozuka desemba 15 kati ya wanajeshi wanaowaunga mkono vigogo hao wawili.

Rais wa Sudani Kusini, Salva Kiir.
Rais wa Sudani Kusini, Salva Kiir. Reuters/Hakim George

“Rais wa Sudani Kusini Salva Kiir anajielekeza Addis Ababa kukutana kwa mazungumzo na kiongozi wa waasi Riek Machar chini ya usimamizi waziri mkuu wa Ethiopia, Hailemariam Desalegn”, amesema waziri wa mambo ya kigeni wa Sudani Kusini, Barnaba Maria kwenye uwanja wa ndege wa Juba, muda mchache kabla ya rais Salva Kiir kujielekeza Ethiopia.

Viongozi hao wawili wamekua wakishawishiwa na jumuiya ya kimataifa, hususan Marekani na Umoja wa Mataifa, wakihofia kutokea kwa mauaji ya kimbari nchini Sudani Kusini.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.