Pata taarifa kuu
MISRI-Usalama

Mkuu wa kikosi cha kuzima vujo nchini Misri auawa

Afisa wa ngazi ya juu wa cheo cha jenerali katika jeshi la Misri ameuawa mapema leo asubuhi katika shambulio la bomu liliyotegwa ndani ya gari lake mjini Cairo. Shambulio hilo limetokea katika mtaa ulioko mashariki mwa mji wa Cairo.

Abdelfatah al-Sissi, ambae atagombea kiti cha urais nchini Misri katika uchaguzi utakaofanyika may 26 na 27
Abdelfatah al-Sissi, ambae atagombea kiti cha urais nchini Misri katika uchaguzi utakaofanyika may 26 na 27 AFP/EGYPTIAN TV
Matangazo ya kibiashara

Shambulio hilo limekua likimlenga, kwa mujibu wa viongozi wa polisi, brigadia jenerali Ahmedi Zaki, mkuu wa kikosi cha kuzima vujo, kikosi ambacho kimekua mstari wa mbele kwa kukabiliana na wafuasi wa rais aliepinduliwa madarakani Mahamed Morsi.

Ni shambulio la tano kwa muda wa juma moja dhidi ya polisi. Brigadia jenerali Ahmedi Zaki ni afisa wa wa tatu kuuawa tangu mwanzoni mwa mwaka katika mashambulizi yanayodaiwa kutekelezwa na makundi ya wanamgambo wa kislamu wenye silaha, ambao wanadai kua na mafungamano na kundi la al-Qaïda, wakibaini kwamba wanajilipiza kisase dhidi ya mashambulizi yaliyotekelezwa na vikosi vya usalama dhidi ya wafuasi wa Morsi, rais wa kwanza aliechagulia kidemokrasia nchini Misri.

Tangu rais Morsi alipopinduliwa madarakani na kukamatwa na jeshi julai 3, waandamanaji 1400 wa kislamu waliuawa na polisi au na jeshi, ambapo 700 waliuawa kwa siku moja ya tarehe 14 ogasti katika mji wa Cairo, huku zaidi ya wafuasi wake 15.000 wakikamatwa na mamia kuhukumiwa kifungo cha maisha jela katika kesi iliyoitishwa na kusikilizwa kwa haraka haraka.

Wakati huohuo, mashambulizi ya kujilipua na mengine ya kuviziya yaliongezeka nchini Misri yakilenga polisi na jeshi.

Hali iliyojiri nchini Misri, wakati wa maandamano ya wafuasi wa Mohamed Morsi novemba 29 mwaka 2103, huku polisi ikijaribu kuzima maandamano hayo.
Hali iliyojiri nchini Misri, wakati wa maandamano ya wafuasi wa Mohamed Morsi novemba 29 mwaka 2103, huku polisi ikijaribu kuzima maandamano hayo. AFP PHOTO/MAHMOUD KHALED

Serikali iliyowekwa na kuongozwa na jeshi limebaini kwamba zaidi ya askari polisi 250, takriban wanajeshi 190 na zaidi ya raia 60 walipoteza maisha katika mashambulizi hayo, ambayo serikali imewahusisha wafuasi wa chama cha Mohamed Morsi cha udugu wa kislamu “Muslim Brotherhood”, na baadae kutangaza chama hicho kwamba ni kundi la kigaidi.

Aprili 2, mashambulizi matatu ya mabomu mjini Cairo yalimuua afisa wa juu wa cheo cha jenerali katika polisi na kuwajeruhi watu watano, akiwemo afisa wa cheo cha jenerali, ambae ni mshauri kwenye wizara ya mambo ya ndani na afisa mwengine wa cheo cha kanali.

Kundi la wanamgambo wakislamu la Ajnad Misr ( wanajeshi wa Misri), ambalo halifahamiki sana lilikiri kuhusika na mashambulizi hayo, huku likitishia kujilipiza kisase kwa kuanzisha kampeni ya kukamatwa kwa wanawake na wasichana wa Misri.

Lakini mashambulizi mengi ya kujilipua na mengine ya kuvizia yaliyotekelezwa tangu julai 3, yalidaiwa kutekelezwa na kundi la Ansar Beït al-Maqdess, lenye mafungamano na kundi la al- Qaïda, ambalo linaendesha harakati zake katika milima ya Sinaï, ambako imekua ikiishambulia Israel kwa roketi.

Shambulio hili la leo linakuja siku tisa baada ya kiongozi wa zamani wa majeshi, Abdel Fattah al-Sissi alie mng'atua madarakani Morsi, kutnagaza rasmi kugombea kwenye uchaguzi wa urasi unaopangwa kufanyika may 26 na 27, ambae aliahidi kushinda uchaguzi huo.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.