Pata taarifa kuu
UN-MALI

UN iko tayari kupatishia uwezo vikosi vya Usalama vya Mali

Umoja wa Ulaya hapo jana umetangaza kuongeza nguvu zaidi kwa vikosi vya polisi na jeshi nchini Mali, ikiwa ni operesheni ya pili kufanywa na umoja wa Ulaya nchini humo kudhibiti hali ya usalama dhidi ya kitisho cha makundi ya kiislamu. 

Wanajeshi wa Mali wakipiga doria
Wanajeshi wa Mali wakipiga doria AFP/JOEL SAGET
Matangazo ya kibiashara

Mkuu wa sera za mambo ya nje wa Umoja wa Ulaya, Catherine Ashton amethibitisha Umoja huo kupitia mawaziri wake wa mambo ya kigeni wanaokutana mjini Brussels, kuidhinisha operesheni ya pili ya umoja huo kwa kutoa mafunzo zaidi kwa vikosi vya Mali.

Katika hatua nyingine akiwa ziarani nchini Senegal, rais wa Mali, Ibrahim Boubacar Keita ameishukuru nchi hiyo kwa kushiriki mchakato wa upatikanaji wa amani nchini mwake, na kuongeza kuwa bado anaunga mkono mazungumzo ya kitaifa nchini mwake.

Rais Keita amesema kuwa ni kwa njia ya mazungumzo na maridhiano ya kitaifa ndiyo yatakayoleta amani nchini Mali na hasa kwenye maeneo ya kaskazini mwa nchi hiyo ambako kunashuhudiwa mgawanyiko bado.

Katika kuunga mkono juhudi za rais wa Mali, Umoja wa Ulaya umetangaza kuongeza muda wa operesheni zake nchini humo mpaka tarehe 28 ya mwezi May mwaka 2016 ambapo wanajeshi wake 560 watasalia nchini humo kutoa mafunzo.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.