Pata taarifa kuu
DRCONGO-NORWAY

Tjostolv Moland mfungwa raia wa Norway akutwa na umauti katika jela kuu jijini Kinshasa

Serikali ya DRCongo kupitia waziri wake wa habari akiwa pia msemaji wake Lambert Mende Omalanga, amesema uchunguzi umeanzishwa ili kubaini kiini cha kifo cha mfungwa huyo huyo raia wa Norway ambaye anashukiwa huenda kajiua mwenyewe. Taarifa za kifo cha Tjostolv Moland zilifahamsihwa na Waziri wa mambo ya nje wa Norway Espen Barth Eide wakati wa mkutano na vyombo vya habari.

Tjostolv Moland, wakati wa uhai wake
Tjostolv Moland, wakati wa uhai wake
Matangazo ya kibiashara

Akizungumza na wanahari habari nchini humo waziri huyo amesema walipokea taarifa hiyo kutoka jijini Kinshasa kuhusu kifo cha Tjostolv Moland ambaye alikutwa amekufa katika chumba chake. Hata hivyo waziri huyo hakutowa maelezi zaidi kuhudu tukio hilo.

Moland pamoja na rafiki yake Joshua French ambao wote ni wanajeshi wa zamani, kesi yao ilianza kusikilizwa mwaka 2009 kwa tuhuma za kuhusika katika mauaji ya dereva wa gari walilokuwa wamekodi, tuhuma ambazo walikana na kudai kuwa dereva huyo aliuawa na majambazi.

Moland na Joshua French ambae pia anauraia wa Uingereza walithibitisha kuwa walikwenda nchini DRCongo kwa dhamira ya kuanzisha kampuni ya ulinzi. Walihukumiwa mwaka 2010 kwa kosa la mauaji na kusudia la kuua pamoja pia na ujasusi na kushiriki katika uhalifu.

Wakati wa hukumu hiyo, Moland aliekuwa na umri wa miaka 32, pamoja na French mwenye umri wa miaka 31 walimuandikia risala rais wa jamuhuri na kumuomba kubadili kifungo cha kifo hadi kifungo cha maisha jela, hukumu ambayo wangeliweza kwenda kumalizia nchini Norway.

Viongozi wa Norway walijaribu kujadiliana na serikali ya DRCongo juu ya kuwasafirisha wafungwa hao.

Vijana hao wawili walikuwa wamehukumiwa kifungo cha kunyongwa jijini Kinshasa kabla ya hukumu hiyo kuahirishwa kutokana na dosari zilizo ikumba kesiu hiyo kwenye mahakama kuu ya kijeshi kabla ya kusilizwa tena mwaka 2010 na kutolewa hukumu ya kifo.

Kiongozi mmoja nchini alisema kwamba Agosti mwaka 2011, vijana hao walijaribu kutoroka, jambo ambalo linakanushwa vikali na mawakili watetezi.

Kwa mujibu wa waziri wa Mambo ya nje wa Norway, mara tu baada ya kuripotiwa kifo cha Moland, serikali ya nchi hiyo imemtuma mjumbe wake jijini kinshasa.

Hakuna utekelezwaji wa hukumu ya kifo uliofanyika tangu ujio wa rais joseph Kabila madarakani mwaka 2001, ambapo makosa makubwa yamekuwa yakigeuka kuwa kifungo cha maisha jela.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.