Pata taarifa kuu
ZIMBABWE

Wagombea urais waendelea kujinadi kuelekea uchaguzi mkuu wa Zimbabwe

Mahasimu wakuu wa kisiasa nchini Zimbabwe Rais Robert Mugabe na Waziri Mkuu Morgan Tsvangirai wameendelea kujinadi katika kampeni za kuwania Urais wa nchi hiyo wakati huu zikiwa zimesalia siku kumi na saba pekee kabla ya wananchi wa Taifa hilo kupigaji kura.

REUTERS/Philimon Bulawayo
Matangazo ya kibiashara

Rais Mugabe akiwa katika kanisa la Marange lililopo mashariki mwa mji mkuu Harare amewataka wapiga kura kutoichagua MDC kwa madai kuwa inataka kurejesha wakoloni katika Taifa hilo.

Naye Waziri Mkuu Tsvangirai akiwa katika mji wa Mutare amewahimiza wapiga kura kutoirudisha madarakani ZANU PF iliyoongoza kwa miaka 33 bila kuwanufaisha wananchi wa Taifa hilo.

Tsvangirai ameahidi kuweka uwazi katika mikataba ya madini ya almasi ambayo ndiyo rasilimali kuu ya uchumi wa Taifa hilo, huku pia akiahidi kutumia fedha zitokanazo na madini hayo kuboresha maslahi ya walimu, wanajeshi na pia kuunda nafasi mpya za ajira kwa vijana.

Uchaguzi huu unatarajiwa kuhitimisha muda wa serikali ya muungano kati ya chama tawala ZANU-PF na chama kikuu cha upinzani MDC iliyoundwa mara baada ya machafuko ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2008.

Kwa mujibu wa katiba ya sasa ya Zimbabwe, Mugabe anayo nafasi ya kuongoza Taifa hilo kwa kipindi cha muongo mmoja ujao endapo atachaguliwa kwa ridhaa ya wananchi wa Taifa hilo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.