Pata taarifa kuu
Zambia

Chama kilichotawala zamani nchini Zambia chafutwa kwa kushindwa kulipa Ada ya usajili

Chama kilichotawala zamani nchini Zambia cha MMD kimeondolewa kwenye orodha ya vyama vya Siasa kwa kushindwa kulipa Ada ya usajili ambapo hivi sasa Chama hicho kinaelekea kunyang'anywa viti vyake vya Ubunge, Msajili wa Vyama nchini humo amethibitisha.

Wafuasi wa Chama cha MMD kilichofutwa na Msajili wa vyama
Wafuasi wa Chama cha MMD kilichofutwa na Msajili wa vyama
Matangazo ya kibiashara

Vyama vya siasa vinatakiwa kulipa ada ya Usajili kila Mwaka lakini Chama cha MMD hakijalipa ada yake tangu mwaka 1993 na sasa kinadaiwa kiasi cha dola za kimarekani 74,300.
 

Msajili Mkuu wa Vyama, Clement Andeleki amesema amekifuta chama hicho kutoka kwenye Orodha ya Vyama vya siasa nchini Zambia kwa mujibu wa Sheria.
 

Uamuzi wa Ndeleki pia utaathiri nafasi 53 za Ubunge ndani ya Bunge la Zambia nafasi zinazoshikiliwa na MMD.
 

Ndeleki amesema atamjulisha Spika wa Bunge Patrick Matibini uamuzi uliofikiwa
Chama cha MMD kilichoongoza tangu Mwaka 1991 kilishindwa katika kinyang'anyiro cha Urais na chama cha Patriotic Front cha Rais Michael Sata kikachukua ushindi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.