Pata taarifa kuu
DRC-UMASIKINI-UCHUMI-SIASA

DRC: Felix Tshisekedi atoa ahadi mpya ya kupambana na vita dhidi ya umaskini

Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Felix Tshisekedi Tshilombo, amehidi wananchi wake kuwa yuko tayari kupambana dhidi ya umaskini uliokithiri nchini humo.

Félix Tshisekedi anataka kuchukua hatua katika wilaya 145 za DRC kwa kupambana dhidi ya umasikini uliokithiri.
Félix Tshisekedi anataka kuchukua hatua katika wilaya 145 za DRC kwa kupambana dhidi ya umasikini uliokithiri. © ISSOUF SANOGO / AFP
Matangazo ya kibiashara

Kauli hiyo inakuja wakati bajeti yake ya kwanza haijawasilishwa bungeni. Rais Tshisekedi ameahidi kuwaondoa raia milioni 20 wa Congo kutoka kwenye umaskini au umaskini uliokithiri katika miaka mitano ijayo. Idadi hii ni robo ya wakaazi wanaokadiriwa nchini DRC. Rais Felix Tshisekedi ametoa hotuba hiyo mbele ya wanadiplomasia katika moja ya vitongoji vya Kinshasa.

Rais Tshisekedi ametoa ahadi hiyo kufuatia uchunguzi mkuu wa mwisho wa kitaifa kuhusu umaskini. Uchunguzi huo ulifanywa kwa kuzingatia kupindi kilio kati ya mwaka 2005 na 2012. Kwa wakati mfupi umasikini ulipungua kwa alama nane na kufikia karibu asilimia 63.4. Na tangu wakati huo, hali haijabadilika sana, Rais Tshisekedi amebainisha. Mnamo mwaka 2017, kiwango cha umasikini kilikadiriwa kuwa asilimia 63, na hata 70% vijijini, ameongeza rais wa DRC.

Rais Tshisekedi amesema anataka kuchukua hatua katika wilaya 145, zote za vijijini au zile zilio karibu na miji.Amesema lengo lake ni kuondoa raia milioni 20 kutoka kwenye umaskini au umaskini uliokithiri kwa kipindi hiki. Amesema atajaribu kuboresha miundombinu kwa raia hao na huduma za kijamii na kiuchumi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.