Pata taarifa kuu
UFARANSA-URUSI-UCHUMI

Mshirika wa karibu wa Putin atakiwa kutoa dhamana ya euro milioni 40

Mahakama ya Rufaa ya Aix-en-Provence, nchini Ufaransa, imemtaka Suleiman Kerimov kutoa dhamana ya euro milioni 40 ili kumuachia huru chini ya udhibiti wa mahakama kama sehemu ya kesi ya kujitajirisha kinyume cha sheria, kwa mujibu wa chanzo cha mahakama.

Suleiman Kerimov, mwenye umri wa miaka 51 anatajwa na Forbes kama miongoni mwa matajiri wa kwanza nchini Urusi. Mali yake ilikadiriwa kuwa zaidi ya dola bilioni 7 mwaka 2013.
Suleiman Kerimov, mwenye umri wa miaka 51 anatajwa na Forbes kama miongoni mwa matajiri wa kwanza nchini Urusi. Mali yake ilikadiriwa kuwa zaidi ya dola bilioni 7 mwaka 2013. © REUTERS/Stringer/File Photo
Matangazo ya kibiashara

Mjasiriamali huyo, ambae ni mwakilishi wa Dagestan katika bunge la seneti la Urusi na mshirika wa karibu wa rais wa Urusi Vladimir Putin, alisikilizwa katika kikao cha faragha siku ya Jumanne na majaji wa Mahakama ya Rufaa.

Ofisi ya mwendesha mashitaka iliomba Bw Kerimov kuendelea kuzuiliwa kwa muda, hatua ambayo Suleiman Kerimov anaonekana kuepuka akam atato dhamana ya euro milioni 40, kwa mujibu wa chanzo cha mahakama.

Mnamo Novemba 23, alifanyiwa uchunguzi Nice (Alpes-Maritimes) kwa ukwepaji mkubwa wa kodi na kuwekwa chini ya udhibiti wa mahakama.

Alipigwa marufuku kuondoka sehemu alikowekwa na kutokua na mawasiliano na watu wengine wanaohusishwa katika kesi yake.

Kulingana na chanzo kilio karibu na kesi hiyo, mahakama ya Ufaransa inainachunguza ununuzi wa "majengo ya kifahari ya kifahari kaatika eneo la Côte d'Azur ambapo, jina lake halionekani, hali ambayo ilipelekea kiwango cha kodi kwa Ufaransa kupunguzwa ".

Kituo cha televisheni cha Rossiya 24, kikinukuu chanzo kisichojulikana, kimeripoti kwamba Suleiman Kerimov alikanusha makosa dhidi yake.

Baada ya kukamatwa, serikali ya Urusi kupitia msemaji wa ikulu ya Kremlin ilitangaza kwamba itamsaidi katika utetezi wake.

Suleiman Kerimov, mwenye umri wa miaka 51 anatajwa na Forbes kama miongoni mwa matajiri wa kwanza nchini Urusi. Mali yake ilikadiriwa kuwa zaidi ya dola bilioni 7 mwaka 2013.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.