Pata taarifa kuu
MAREKANI-MEXICO-USHIRIKIANO

Trump kuagiza utozwaji kodi kwa bidhaa kutoka Mexico

Ikulu ya Marekani inasema rais Donald Trump ataagiza utozwaji zaidi wa kodi wa bidhaa vinavyoingia Marekani kutoka Mexico, na fedha zitazopatikina zitatumiwa kujenga ukuta kati ya nchi hizo mbili.

Donald Trump mbioni kuagiza utozwaji zaidi wa kodi wa bidhaa vinavyoingia Marekani kutoka Mexico, na fedha zitazopatikina zitatumiwa kujenga ukuta kati ya nchi hizo mbili.
Donald Trump mbioni kuagiza utozwaji zaidi wa kodi wa bidhaa vinavyoingia Marekani kutoka Mexico, na fedha zitazopatikina zitatumiwa kujenga ukuta kati ya nchi hizo mbili. REUTERS/Jose Luis Gonzalez
Matangazo ya kibiashara

Rais wa Mexico Enrique Pena Nieto ameshtumu hatua ya Trump na hata kusitsiha ziara aliyopanga kwenda Marekani kukutana na rais Trump.

Kama Mexico haiko tayari kugharamia ujenzi wa ukuta, ambao unahitajika, itakuwa bora kufuta mkutano ujao," Rais Donald Trump aliandika kwenye ukurasa wake wa Twitter Jumatano wiki hii. Mwenzake wa Mexico amemjibu. Wakati ambapo alikua anapanga ziara ya kikazi mjini Washington wiki ijayo, Enrique Peña Nieto ametangaza Alhamisi ,pia kupitia Twitter, kwamba anafuta ziara yake ya mjini Washington. "Asubuhi hii nimeiarifu Ikulu ya White House kwamba sintohudhuria mkutano wa kikazi uliopangwa kufanyika Jumanne ijayo pamoja na rais wa Marekani," rais wa Mexico ameandika.

Trump amesema, walikubaliana kusitisha mkutano huo.

Donald Trump alifanya juhudi kubwa za kidiplomasia. Katika hotuba yake kwenye wizara ya usalama wa taifa Jumatano, Januari 25, rais wa Marekani alijizuia na uchokozi wowote ulioshuhudiwa wakati wa kampeni yake ya uchaguzi, amearifu mwandishi wetu mjini Washington, Anne-Marie Capomaccio. Alikuwa makini kwa kusema kwamba wananchi wa Mexico ni marafiki wa Marekani na kwamba ukuta inaotaka kujenga kwenye mpaka na Mexico ni jambo baya kwa nchi hizo mbili. Akiongeza kuwa kwa njia moja au nyingine, Mexico itagharamia ujenzi wa ukuta huo.

Lakini kukataa kwa rais wa Mexico kufadhili ujenzi wa ukuta huo kulisababisha rais Donald trump kupandwa na hasira. Chini ya wiki moja baada ya kuapishwa kwake, Rais wa Marekani anakabiliwa na tukio la kwanza la kidiplomasia.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.