Pata taarifa kuu
CUBA-EU-USHIRIKIANO

Umoja wa Ulaya na Cuba wahitimisha makubaliano ya kisiasa

Jumatatu hii Desemba 12 Umoja wa Ulaya na Cuba walisaini mkataba wa kisiasa, utakaoruhusu makampuni ya Ulaya nchini Cuba ili uchumi wa kisiwa hicho uwe imara.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Cuba, Bruno Rodriguez, akimfumbatia mkono mkuu wa sera za kigeni za Umoja wa Ulaya Ulaya, Federica Mogherini, pamoja na Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Slovakia, Miroslav Lajčák, baada ya kusaini makubaliano ya kisiasa.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Cuba, Bruno Rodriguez, akimfumbatia mkono mkuu wa sera za kigeni za Umoja wa Ulaya Ulaya, Federica Mogherini, pamoja na Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Slovakia, Miroslav Lajčák, baada ya kusaini makubaliano ya kisiasa. REUTERS/Francois Lenoir
Matangazo ya kibiashara

Makubaliano kuhusu mazungumzo ya kisiasa na ushirikiano ni ya kwanza kuwa kuhitimiswa kati ya Umoja wa Ulaya na Cuba na kusainiwa kwake kunaonyesha kuwa hatua kubwa imepigwa katika masuala ya kidiplomasia katika mahusiano baina ya nch hizi mbili tangu kuondolewa vikwazo vya Ulaya dhidi ya kisiwa hicho kilio chini ya utawala wa kikomunisti, mwaka 2008.

"Tumeanza kufungua pamoja ukurasa mpya," amesema Federica Mogherini, msemaji wa sera za kigeni katika Umoja wa Ulaya, wakati wa sherehe za kusaini mjini Brussels akiambatana na Waziri wa mambo ya Nje wa Cuba, Bruno Rodriguez Parrilla.

Akiwasilisha rambirambi za Umoja wa Ulaya kwa kifo cha Fidel Castro, aliyefariki Novemba 25 akiwa na umri wa miaka 90, Federica Mogherini amesema kuwa Ulaya inafufua uhusiano na Cuba wakati ambapo nchi hii imepitia "mabadiliko makubwa ".

Makubaliano hayayanawapa wanadiplomasia wa Ulaya haki ya kuinua sauti kuhusu suala la haki za binadamu moja kwa moja kwa wenzao wa Cuba, na kufanya shinikizo kwa ajili ya mageuzi.

Wakati huo huo, Umoja wa Ulaya, amesema Federica Mogherini, unarudi na mkataba huu kuhusu "msimamo wake wa pamoja" kwa Cuba, uliyopitishwa mwaka 1996, ambapo ulipendekeza haki za binadamu na demokrasia kama sharti katika kuboresha mahusiano ya kiuchumi, katika kile serikali ya Havana iliona kuwa ni kuingiliwa katika masuala yake ya ndani.

Makubaliano haya, Rodriguez amesema, yatawezesha maendeleo ya uhusiano wa kibiashara, kitamaduni, kifedha na kisayansi kati ya Umoja wa Ulaya na Cuba, na yanaonyesha kwamba pande zote mbili zinaweza "kuondokana na tofauti [zao]" kwa kufufua mahusiano yao katika hali ya "kuheshimiana" .

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.