Pata taarifa kuu
AFRIKA KUSINI-ANC-SIASA

Kiongozi mwandamizi wa ANC atoa wito wa kujiuzulu kwa Jacob Zuma

Nchini Afrika Kusini, vita vimetangazwa katika chama tawala cha ANC. Kiongozi wa kundi la wabunge kutoka chama cha ANC, Jackson Mthembu, alitoa wito Jumapili Oktoba 23 wa kujiuzulu kwa kamati tendaji nzima ya chama hiki na Jacob Zuma kuondoka mamlakani.

Rais wa Afrika Kusini, Jacob Zuma, akabiliwa na tuhuma mbalimbali, hku akilaumiwa na baadhi ya maafisa waandamizi wa chama chake kushindwa kutafutia ufumbuzi hali ya sintofahamu inayojiri katika chama hiki.
Rais wa Afrika Kusini, Jacob Zuma, akabiliwa na tuhuma mbalimbali, hku akilaumiwa na baadhi ya maafisa waandamizi wa chama chake kushindwa kutafutia ufumbuzi hali ya sintofahamu inayojiri katika chama hiki. REUTERS/Siphiwe Sibeko
Matangazo ya kibiashara

Msimamo huu umetolewa wakati ambapo hali ya sintofahamu inaendelea kushuhudiwa katika chama hiki cha hayati Tata Nelson Madiba Mandela. Kwa upande mmoja, Waziri wa Fedha Pravin Gordhan anashtumiwa makosa ya udanganyifu, lakini wengi wanaona kuna mkono wa serikali, iliyomchawishikuchukua udhibiti wa fedha za umma. Kwa upande mwingine, ripoti ya mwisho ya mpatanishi wa zamani wa Jamhuri Thuli Madonsela ni sababu ya Rais Jacob Zuma, kutaka kuzuia kutolewa kwa ripoti hii.

Kwa nyuma: mazoea questionable utafutaji juu ya hali, na mahusiano machafuko na Rais Zuma tajiri Hindi industrialist familia Gupta. Matukio yote haya kuwa kuchonga kina kosa mistari ndani ya ANC dhaifu kisiasa baada ya kushindwa kwake uchaguzi katika uchaguzi wa manispaa wa Agosti.

Kiongozi wa kundi la wabunge ameuvunja mwiko katika mahojiano mawili mfululizo siku ya Jumapili. lisema ili kuokoa chama, ni kamati zote za chama cha ANC zinapaswa kurejelewa. Jackson Mthembu hakuficha maneneo yake: "sote tunapaswa kujiuzulu , na yeye akiwemo" na hali hii inamhusu Rais Jacob Zuma, Makamu rais Cyril Ramaphosa na Katibu Mkuu wa chama cha ANC Gwede Mantashe.

Bw Mthembu anawatuhumu viongozi hawa kuwa 'walikigawanya chama na kusababisha hali ya mtafaruku ndani ya nchama hiki'.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.