Pata taarifa kuu
KOMBE LA DUNIA BRAZIL 2014

Wasifu wa timu ya Taifa ya Brazil

Imeshiriki kombe hili mara 19, imechukua mara 5, nafasi ya 6 FIFA.Historia kwenye kombe la Dunia la FIFA.Nchi ya Brazil ndio muandaaji wa fainali za kombe la dunia kwa mwaka huu wa 2014, timu yake ya taifa kwa mwaka huu inapewa nafasi ya kushinda kombe hili. Brazil ni maarufu kama “Samba Boys” kutokana na aina ya mchezo wake, na ndio timu pekee ambayo imeshiriki katika kila fainali za kombe la dunia toka lilipoanza.Timu hii inahistoria ya kipekee kwa kuwa imeshalitwaa kombe hili mara tano, mwaka 1958, 1962, 1970, 1994 na 2002.

Wachezaji wa timu ya taifa ya Brazil wakishangilia moja ya goli walilofunga
Wachezaji wa timu ya taifa ya Brazil wakishangilia moja ya goli walilofunga fifa.com
Matangazo ya kibiashara

Kundi ililopo.

Brazili iko kwenye kundi A kwenye michuano ya mwaka huu, kundi lake linaundwa na timu ya taifa ya Croatia, Mexico na vinara wa Afrika wa siku nyingi timu ya taifa ya Cameroon. Kundi hili linatajwa kuwa lakipekee kutokana na timu zinazounda kundi lake kama vile Mexico na Croatia ambazo ni timu ngumu kufungika.

Wachezaji wa kuangaliwa.

Mshambuliaji wake Neymar, tayari ametajwa kama kinda ambaye atawika na timu yake ya taifa kutokana na uwezo wake wa kupachika mabao na chenga za maudhi uwanjani. Pia yuko mchazji Robinho anayekipiga na klabu ya Santos, Dani Alves anayekipiga na klabu ya Barcelona, yupo pia mlinda mlango mkongwe, Julio Cesar.

Benchi la ufundi.

Timu ya taifa ya Brazil inaongozwa na kocha Luiz Felipe Scolar.

Mafanikio kwenye kombe la dunia la FIFA.

Ilifanya vizuri kwenye michuano ya kombe la dunia la mwaka 1958 nchini Sweeden, Chile mwaka 1962, Mexico mwaka 1970, Marekani mwaka 1994, Korea na Japan mwaka 2002 ambapo walikuwa mabingwa. Pia imefanya vizuri kwenye michuano ya kombe la dunia la FIFA kwa vijana walio chini ya umri wa miaka 20 ambapo mwaka 1983 ilishiriki kule nchini Mexico, pia ile iliyofanyika kwenye nchi za kisovite mwaka 1985, Australia mwaka 1993, falme za kiarabu mwaka 2003 ambapo walikuwa mabingwa.

Wachezaji waliovuma.

Garrincha, Pele, Bebeto na Ronaldo De Lima.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.