Kusikiliza Pakua Podcast
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 04h30 - 05h00 TU
    Uchambuzi na makala 25/01 04h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 05h30 - 06h00 TU
    Uchambuzi na makala 25/01 05h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 15h00 - 16h00 TU
    Uchambuzi na makala 25/01 15h00 GMT
Ili Kufurahia kikamilifu maudhui ya multimedia yetu, unahitaji kuwa na Plugin iliyowekwa kwenye kompyuta yako Ili kuingia, unahitaji kuruhusu cookies zote kwa kuseti vizuri Ili kutembelea mtandao, tovuti ya RFI inaenda sambamba na Internet Explorer 8 na + Firefox 10 na +, Safari 3 na +, Chrome 17 na + nk
E.A.C

Mvutano kati ya Burundi na Rwanda waendelea

media Mamlaka ya Burundi imethibitisha shambulio dhidi ya jeshi lake katika msitu wa Kibira, huku ikinyooshea kidole Rwanda, Novemba 17, 2019. Google Maps

Shambulio la kijeshi dhidi ya vikosi vya Burundi mwezi uliopita katika eneo la mpaka na Rwanda limezidisha hali ya mvutano wa moja kwa moja baina ya nchi hizo mbili. Serikali ya Giteg imeituhumu Kigali kuhusika na kile ilichokiita uvamizi wa kijeshi.

Shambulio hilo lilifanyika usiku wa Novemba 16 katika kijiji cha Twinyoni kwenye umbali wa kilometa 100, Kaskazini mwa mji mkuu Bujumbura ndani ya msitu wa Kibira kilometa 5 na mpaka na Rwanda.

Kwa mujibu wa manusura, washambuliaji walikuwa wamevalia nguo zisizoshika risase pamoja na miwani ya kuona usiku

Duru za serikali zilieleza kwamba wanajeshi wanane ndio waliopoteza maisha, lakini kiongozi mmoja wa kijeshi pamoja na ndugu wa waliopoteza maisha ikathibitisha idadi ya wanajeshi 19 huku wengine 19 wakijeruhiwa.

Hili lilikuwa ni moja miognoni mwa mashambulizi makubwa kufanywa na kaundi la waasi katika ardhi ya Burundi tangu mwaka 2015 wakati rais wa sasa Pierre Nkurunziza alipoamuwa kuwania muhula wa 3 hatuaa iliozua mzozo wa kisiasa na kuichumi na umwagaji wa damu.

Kwanza kabisa Bujumbura iliwanyooshea kidole kundi la waasi ambao hata hivyo haikuwataja jina waliotokea nchini Rwanda, kabla ya kubadili baadae na kulituhumu jeshi la Rwanda bila hata hivyo kuonyesha ushahidi wa kutosha, na tayari imewasilisha mashtaka mbele ya Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Mashtaka kama hayo pia yamewasilishwa kwa Jumuiya ya nchi za Ukanda wa Afrika mashariki ICGLR ambayo imetuma ujumbe wake nchini Burundi na Rwanda kwa ajili ya kwenda kufanya uchunguzi.

Serikali ya Kigali kupitia Waziri wake wa Mambo ya Nje Olivier Ntuhungirehe imetupia mbali tuhuma dhidi yake, na kueleza kwamba hakuna mtu yeyote yule alieshambulia Burundi akitokea nchini Rwanda na kuongeza kuwa hizi ni tuhuma ambazo zimekuwa zikitolewa sasa ni miaka minne na hazina ukweli ndani yake.

Duru za kuaminika zinaeleza kwamba serikali ya Bujumbura inasogeza vikosi vyake zaidi eneo la mpaka wake na Rwanda.

Kuhusu mada hiyo hiyo
 
Samahani, mwunganisho na sava umeshindikana