Kusikiliza Pakua Podcast
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 04h30 - 05h00 TU
    Uchambuzi na makala 12/12 04h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 05h30 - 06h00 TU
    Uchambuzi na makala 11/12 05h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 15h00 - 16h00 TU
    Uchambuzi na makala 11/12 15h00 GMT
Ili Kufurahia kikamilifu maudhui ya multimedia yetu, unahitaji kuwa na Plugin iliyowekwa kwenye kompyuta yako Ili kuingia, unahitaji kuruhusu cookies zote kwa kuseti vizuri Ili kutembelea mtandao, tovuti ya RFI inaenda sambamba na Internet Explorer 8 na + Firefox 10 na +, Safari 3 na +, Chrome 17 na + nk
Habari mpya kabisa
  • Macron aahirisha mkutano wa kilele wa Pau kuhusu Sahel hadi mwanzoni mwa mwaka 2020 kwa sababu ya shambulio nchini Niger (Elysee)
E.A.C

Polisi ya Tanzania yakana 'kumteka' mwanahabari Erick Kabendera

media Kamanda wa polisi kanda maalumu ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa akizungumza na wanahabari leo Julai 30 mwaka 2019 Jijini Dar es salaam, Tanzania RFI Kiswahili/Fredrick Nwaka

Polisi ya Tanzania imekana kumteka mwanahabari Erick Kabendera na kuainisha kwamba mwandishi huyo wa habari anashikiliwa na vyombo vya usalama na anahojiwa kuhusu uhalali wa uraia wake.

Kamanda Wa Kanda Maalumu Lazaro Mambosasa anasema Polisi ilimpa wito Wa kumwita kwa Mahojiano lakini Hakufika.

"Huyu mtu hajatekwa, anashikiliwa na yupo kituoni Hapa, tunachunguza Uraia wake kwa kushirikiana na uhamiaji,"

Hata Hivyo Mambosasa hajaeleza kwa kina kwa nini jeshi hilo linachunguza uraia Wa Mwanahabari huyo na Kusema akisema huenda akaharibu uchunguzi.

Amewataka Watanzania kuepuka Habari zinazoweza kuzua taharuki.

Erick Kabendera amewahi kuandikia magazeti kadhaa ya ndani na nje ya Tanzania na ni mmoja wa wanahabari  wanaoheshimika kwa kazi zao.

Kuhusu mada hiyo hiyo
 
Samahani, mwunganisho na sava umeshindikana