Pata taarifa kuu
BURUNDI-COMESA-UCHUMI

Mkutano wa 20 wa Comesa wamalizika Zambia, Burundi yashtumu

Mkutano wa 20 wa viongozi wa soko la pamoja la mashariki na kusini mwa Afrika Comesa umemalizika jijini Lusaka nchini Zambia.Ni mkutano ambao ulikuwa umepangwa kufanyika jijini Bujumbura nchini Burundi.

Lusaka, mji mkuu wa Zambia ambako ulifanyika mkutano wa kilele wa Comesa.
Lusaka, mji mkuu wa Zambia ambako ulifanyika mkutano wa kilele wa Comesa. © Getty Images/Stuart Fox
Matangazo ya kibiashara

Serikali ya Burundi ilisusia mkutano huo wa kilele wa viongozi wa soko la pamoja la mashariki na Kusini mwa Afrika (Comesa) ambao ulianza tangu jJumatano na kutamatika Alhamisi wiki hii jijini Lusaka nchini Zambia kwa madai kwamba umefanyika kinyume cha sheria.

Mkutano huo ulikuwa umepangwa kufanyika jijini Bujumbura kabla ya kuahirishwa kupelekwa huko Lusaka katika kile ambacho serikali ya Burundi imesema kupitia naibu msemaji wa rais wa Burundi Alain Diomede Nzeyimana kuwa hapakuwa na sababu za msingi za mkutano huo kutofanyika jijini Bujumbura.

Msemaji huyo wa rais jijini Bujumbura amesema uamuzi wa kuahirishwa kwa mkutano huo kufanyika jijini Bujumbura ilitakiwa kuchukuliwa na viongozi watatu akiwemo wa Burundi, wa Ethiopia na wa Madagascar ambo ni wajumbe wa ofisi ya mkutano wa kilele wa Comesa, lakini sivyo ilivyofanyika.

Alain Diomede Nzeyimana amesema wajumbe katika mkutano huo walikwenda mjini Lusaka kwa faida zao binafasi.

Mwezi Mei mwaka huu katibu mkuu wa Comesa aliamua kuhamisha mkutano huo wa kilele kutoka Bujumbura hadi Lusaka kutoka na kile kilichodaiwa kuwa ni kwa sababu za kiusalama. Jambo ambalo serikali ya burundi imesisitiza ni ukosefu wa heshima kwa taifa huru.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.