Pata taarifa kuu
SUDANI KUSINI-UN-HAKI

Askari wa Nepal washtumiwa kuwabaka watoto Sudan Kusini

Wanajeshi wa kulinda amani kutoka Nepal wanakabiliwa na madai ya kuwabaka watoto nchini Sudan Kusini. Msemaji wa Umoja wa Mataifa Stephane Dujarric amesema tayari Umoja wa Mataifa umetuma watalaam wake kwenda kuchunguza ukweli wa madai hayo.

Wanajeshi wa kulinda amani nchini Sudan Kusini.
Wanajeshi wa kulinda amani nchini Sudan Kusini. AFP/Charles Atiki Lomodong
Matangazo ya kibiashara

Haijaelezwa kwa undani idadi ya wanajeshi waliohuska katika madai hayo. Hii sio mara ya kwanza kwa wanajeshi wa Umoja wa Mataifa ncini Sudan Kusini kushtumiwa kwa kuhusika katika madai haya kwa watoto na wanawake.

Wanajeshi wa kulinda amani wamekua wakishtumiwa madai ya kuwabaka watoto katika nchi mbalimbali, hasa barani Afrika.

Hivi karibuni walinda amani kutoka DRC, walifukuzwa nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati kwa madai kama hayo.

Umoja wa Mataifa unasema kuna madai 40 ya ukatili na unyanysaji wa kingono ambayo inayafanyia kazi.

Umoja wa Mataifa umesema utaendelea kufuatilia na kuchukua hatua huku ukiyafanyia kazi madai yote ya unyanyasaji na ukatili wa kingono kwenye mfumo wa Umoja wa mataifa kwa kuzingatia mkakati wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa wa uwazi dhidi ya madai hayo.

Hayo yameelezwa na msemaji wa Umoja wa Mataifa hii leo Stephane Dujarric akizungumza na waandishi wa Habari mjini New York Marekani na kuongeza kuwa tangu Oktoba Mosi hadi Desemba 31 mwaka 2017 Umoja wa Mataifa umepokea madai 40 dhidi ya mashirika yake na watendaji wadau, ingawa amesema siyo madai yote yaliyothibitishwa na mengi bado yako katika hatua za mwanzo za tathimini na kwamba kati ya madai hayo 40, Madai 15 yameripotiwa kutoka kwenye operesheni za ulinzi wa amani na yote yameingizwa katika orodha ya maadili na nidhamu kadri yalivyokuwa yakija.

Ameongeza kuwa kati ya madai hayo 40 , madai 13 yametajwa kuwa ni ya ukatili wa kingono, 24 ya unyanyasaji wa kingono na matatu hayajulikani ni ya nini.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.