Pata taarifa kuu
BURUNDI-HRW-HAKI

Human Right Watch yaituhumu serikali ya Burundi kukandamiza wapinzani

Shirika la Kimataifa la Kutetea haki za Binadamu la Human Rights Watch limewashtumu maafisa wa usalama nchini Burundi kwa kuendelea kuwauawa, kuwapiga, kuwakamata na kuwazuia wapinzani wanaopinga mchakato wa kuibadilisha Katiba mwezi ujao.

Rais wa Burundi, Pierre Nkurunziza akikagua gwaride la heshima la askari wake wakati wa maadhimisho ya miaka 54 ya uhuru wa Burundi.
Rais wa Burundi, Pierre Nkurunziza akikagua gwaride la heshima la askari wake wakati wa maadhimisho ya miaka 54 ya uhuru wa Burundi. Onesphore Nibigira/AFP
Matangazo ya kibiashara

Human Rights Watch inasema tangu mwezi Desemba mwaka uliopita, watu 19 wapinzani 19 wa serikali wameteswa na maafisa wa usalama nchini humo.

Ripoti hii inakuja wakati huu, viongozi wa Umoja wa Mataifa na Umoja wa Afrika wakitoa wito kwa serikali na upinzani kumaliza tofauti zao kwa ajili ya amani ya taufa hilo.

Tangu Desemba 12 wakati rais Pierre Nkurunziza alipotangaza kufanyika kura ya maoni, maafisa wa serikali na wanachama wa kundi la la vijana wa chama tawala CNDD-FDD (Imbonerakure) wametumia vitisho na ukandamizaji kuhakikisha kura zinaelekezwa kumfaidisha rais Nkurunziza. Kura hiyo itamuwezesha rais huyo wa Burundi ambaye tayari anatumikia muhula uliyo na utata, kuurefusha utawala wake hadi mwaka 2034.

Mateso haya yanajumuisha kumpiga na kumuua mtu mmoja aliyekosa kuthibitisha kuwa amejisajili kupiga kura, kuuwawa kwa watu waliyozuiliwa na polisi pamoja na kamata kamata inayoendelea hasa kwa wanachama wa chama cha upinzani cha FNL.

Aidha duru za kuaminika zimeliambia shirika la Human Rights Watch kwamba visa hivyo vya udhalilishaji vimekuwa vikiendelea nchi nzima. .

Tangu mwaka 2015 wakati mgoggoro wa kisiasa ulipoanza nchini Burundi, baada ya rais Nkurunziza kutangaza kuwania muhula mwengine madarakani, vyombo huru vya habari nchini humo na mashirika yasio ya kiserikali vimefungiwa, huku zaidi ya watu 397,000 wakiitoroka nchi hiyo, shirika la Human Rights Watch lilisema.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.