Pata taarifa kuu
TANZANIA-WANAHABARI

Tanzania: Sheria ya Huduma ya vyombo vya Habari yapingwa Mahakamani

Wanahabari na wanaharakati nchini Tanzania wamekwenda Mahakamani kupinga Sheria ya Huduma ya vyombo vya Habari  kwa kile wanachosema, itatishia uhuru wa wanahabari nchini humo.

Picha sehemu ya magazeti ya Tanzania
Picha sehemu ya magazeti ya Tanzania RFI Kiswahili
Matangazo ya kibiashara

Kesi hii imewasilishwa katika Mahakama ya Afrika Mashariki inayosghulikia Haki mjini Arusha, Kaskazini mwa nchi hiyo.

Wanaharakati hao wanasema sheria hiyo mpya inaminya uhuru wa vyombo vya Habari hasa baada ya serikali kuyafungia magazeti kadhaa kwa kuikosoa serikai.

Baraza la Wanahabari nchini humo na watetezi wa haki za binadamu wanasema kuna baadhi ya vifungu katika  sheria hiyo vinavyowanyima wanahabari haki na uhuru wa kuchapisha taarifa mbalimbali.

Aidha, wanapinga  kifungo cha sheria hiyo kinachowataka wanahabari kupewa kibali cha kufanya kazi na kuwepo kwa mamlaka inayoweza kuwazuia wanahabari kupewa kibali hicho.

Juhudi za wadau wa sekta ya Habari nchini humo kutaka kupewa muda zaidi kutoa maoni yao kuhusu sheria hii mpya kabla ya kutiwa saini, hazikuzaa matunda.

Serikali nchini humo imekuwa ikisema sheria hiyo ni nzuri kwa sababu inasaidia kuimarisha  sekta ya unahabari katika taifa hilo la Afrika Mashariki.

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.