Pata taarifa kuu
TANZANIA-SIASA

Mwanasiasa wa serikali nchini Tanzania ajiuzulu ubunge na kuhamia upinzani

Aliyekuwa Waziri wa Maliasili na Utalii katika serikali ya awamu ya nne nchini Tanzania, Lazaro Nyalandu ametangaza kujivua uanachama katika Chama tawala cha CCM.

Lazaro Nyalandu mwanasiasa na waziri wa zamani aliyehamia upinzani
Lazaro Nyalandu mwanasiasa na waziri wa zamani aliyehamia upinzani twitter.com/LazaroNyalandu?
Matangazo ya kibiashara

Kabla ya kuchukua uamuzi huo Nyalandu amekuwa Mbunge wa Jimbo la Singida Kaskazini, Katikati mwa Tanzania tangu mwaka 2000.

Kiongozi huyo ametoa sababu mbalimbali ikiwamo kutoridhishwa na mwenendo wa kisiasa pamoja na ukiukwaji wa haki za binadamu.

Pia mbunge huyo ambaye alikuwa Waziri wakati wa utawala wa Rais Jakaya Mrisho Kikwete kukithiri kwa vitendo vya dhuluma wanavyofanyiwa baadhi ya watanzania na kutokuwepo kwa mipaka ya wazi baina ya mihimili ya serikali kama sababu nyingine zilizomsukuma kuchukua uamuzi wa kujiululu nyadhifa zake.

Uamuzi wa kujivua nyadhifa alizokuwa anazishikilia ikiwemo ya Ubunge, inaliacha wazi Jimbo la Singida Kaskazini ambapo sasa tume ya uchaguzi ya Tanzania NEC italazimika kuitisha uchaguzi mdogo.

Nyalandu alizaliwa miaka 47 iliyopita mkoani Singida na kabla ya kuwa mbunge alifanya kazi mbalimbali nchini Marekani na Tanzania.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.