Pata taarifa kuu
KENYA-UCHAGUZI

Odinga atoa wito kwa wafuasi wake kususia uchaguzi wa urais Kenya

Kiongozi wa muungano wa upinzani nchini Kenya Raila Odinga, Jumatano hii amewataka wafuasi wake kususia uchaguzi wa urais uliopangwa kufanyika Alhamisi hii Oktoba 26 licha ya vurugu na utata wa kisiasa ambao ulishuhudiwa katika kampeni za uchaguzi.

Kiongozi wa muungano wa upinzani nchini Kenya Raila Odinga amesema wataendelea na msimamo wa kupinga uchaguzi kufanyika Alhamisi Oktoba 26, 2017..
Kiongozi wa muungano wa upinzani nchini Kenya Raila Odinga amesema wataendelea na msimamo wa kupinga uchaguzi kufanyika Alhamisi Oktoba 26, 2017.. REUTERS/Baz Ratner
Matangazo ya kibiashara

"Kama hakuna haki kwa watu, hakuna amani kwa serikali," Odinga amewaambia wafuasi wake, katika mkutano mjini Nairobi baada ya kutangazwa kufanyika kwa uchaguzi Alhamisi hii Oktoba 26.

Uchaguzi huu ni kurudiaya uchaguzi wa Agosti 8, ambapo Rais Uhuru Kenyatta aliibuka mshindi lakini matokeo yake yalifutwa na Mahakama Kuu.

Bw. Odinga, ambaye aliamua kujondoa katika kinyang'anyiro hicho akipinga dhidi ya kutokuepo na mageuzi ndani ya Tume ya Uchaguzi, ametangaza kuwa muungano wake wa kisiasa utageuka kuwa vuguvugu la kisiasa. Amesema uchaguzi mpya unapaswa kufanyika ndani ya siku 90.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.