Pata taarifa kuu
UGANDA-MAHAKAMA-UGAIDI

Kiongozi wa kundi la Kiislamu la Tabliq nchini Uganda ahukumiwa maisha jela

Mahakama Kuu nchini Uganda, imempa kifungo cha maisha jela kiongozi wa kundi la Kiislamu la Tabliq Sheikh Mohammad Yunus Kamoga kwa makosa ya kigaidi.

Kiongozi wa kundi la Kiislamu la Tabliq nchini Uganda Sheikh Mohammad Yunus Kamoga nje ya Mahakama jijini Kampala baada ya kuhukumiwa maisha jela
Kiongozi wa kundi la Kiislamu la Tabliq nchini Uganda Sheikh Mohammad Yunus Kamoga nje ya Mahakama jijini Kampala baada ya kuhukumiwa maisha jela Photo by Abubaker Lubowa
Matangazo ya kibiashara

Hii ina maana kuwa, Sheikh Kamoga atasalia jela kwa kipindi chote cha maisha yake.

Mbali na Kamoga, wengine waliopewa adhabu hiyo kali ni pamoja na Sheikh Siraje Kawooya, Sheikh Murta Mudde Bukenya na Sheikh Fahad Kalungi.

Licha ya kupatikana na kosa hilo, Mahakama imewaondoa madai ya kuwauwa viongozi wengine wa Kiislamu Sheikh Mustafa Bahiga, Ibrahim Hassan Kirya miongoni mwa wengine.

Mahakama hiyo ikiongozwa na Jaji Ezekiel Muhanguzi, imeamua pia Kakande Yusufu maarufu kama Abdallah na Sekayaja Abdulsalam maarufu kama Kassim Mulumba wahukumiwe jela miaka 30 kwa makosa hayo ya ugaidi lakini ikaeleza kuwa kifungo chao ni tofauti kwa sababu, wao walikuwa ni wafuasi tu.

Hata hivyo, wakili wao Fred Muwema amesema kuwa, atakataa rufaa.

Mahakama imesema kuwa wafungwa hao wana siku 14 kufanya hivyo.

Wengine walioachiliwa huru baada ya kesi hiyo kukamilika ni pamoja na Amir Kinene, Hakeem Kinene, Abdul Rashid Sematimba, Hamza Kasirye, Twaha Sekitto, Rashid Jingo, Musa Isa Mubiru na Yiga George William.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.