Pata taarifa kuu
TANZANIA-CUBA

Makamu wa rais wa Cuba ziarani nchini Tanzania

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Cuba, Salvador Antonio Valdes Mesa, yuko nchini Tanzania kwa ziara ya siku tatu, ambapo aliwasili nchini humo jana jioni na leo anatarajiwa kukutana na mwenyeji wake rais wa Tanzania.

Makamu wa rais wa Cuba, Salvador Antonio Valdes Mesa akiwa na mwenyeji wake makamu wa rais wa Tanzania Samia Suluhu
Makamu wa rais wa Cuba, Salvador Antonio Valdes Mesa akiwa na mwenyeji wake makamu wa rais wa Tanzania Samia Suluhu Ikulu/Tanzania
Matangazo ya kibiashara

Kiongozi huyo alipokelewa kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere na makamu wa rais Samia Suluhu, ambapo anatarajiwa kuwa nchini kwa siku tatu, na muda mfupi ujao atakuwa na mazungumzo ya faragha na mwenyeji wake rais John Pombe Magufuli.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na ikulu ya Dar es Salaam, imesema kuwa, ziara hii imelenga kuendelea kuimarisha ushirikiano kati ya Tanzanoa na Cuba na hasa katika sekta za elimu, afya, utamaduni, michezo, kilimo, nishati, tekenolojia pamoja na kuangalia maeneo mapya ya uwekezaji.

Mbali na kuwa na mazungumzo na rais Magufulu, makamu wa rais wa Cuba pia atakutana kwa mazungumzo mengine na makamu wa rais Samia Suluhu, kabla ya kukutana na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, kueleza yale waliyozungumza kabla ya kuelekea visiwani Zanzibar .

Cuba na Tanzania zina uhusiano wa kihistoria ambao uliasisiwa na viongozi wa mataifa hayo mawili, aliyekuwa rais wa kwanza wa Tanzania marehemu Julius Nyerere na rais Mstaafu wa Cuba, Fidel Castro, ambapo walishirikiana hata baada ya Marekani kutangaza vikwazo kwa nchi hiyo.

Makamu wa rais Salvador Antonio Valdes Mesa, pia atazuru nchi ya Uganda, DRC, Botswana na Zimbabwe.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.