Pata taarifa kuu
KENYA

Mchakato wa kumtafuta Jaji Mkuu mpya nchini Kenya waanza

Tume ya huduma ya Mahakama nchini Kenya, imeanza zoezi la kumtafuta Jaji Mkuu mpya na rais wa Mahakama ya Juu baada ya kustaafu kwa Willy Mutunga mwezi Juni.

Jengo la Mahakama ya Juu jijini Nairobi
Jengo la Mahakama ya Juu jijini Nairobi Wikipedia
Matangazo ya kibiashara

Nafasi hiyo imewavutia watu sita wengi wao wakiwa Majaji.

Watu hao ni pamoja na Majaji wa Mahakama ya rufaa Alnashir Visram, David Maraga, Roselyn Nambuye na wakili Nzamba Kitonga.

Wengine ni Majaji Smokin Wanjala Jaji wa Mahakama ya Juu na jaji mwingine wa Mahakama kuu Msagha Mbogholi.

Mbali na kumtafuta Jaji Mkuu, Tume hiyo inatarajiwa kujaza nafasi ya Naibu Jaji Mkuu na Jaji mwingine mmoja baada ya Majaji wawili kustaafishwa kwa lazima na Tume ya huduma Mahakama.

Katiba ya Kenya inaeleza kuwa zoezi la kuwahoji ni lazima lifanywe wazi na wakenya kushirikishwa kikamilifu katika muda wote wa mahojiano hayo.

Zoezi hili ni muhimu sana kwa nchi hiyo inayoelekea kwenye Uchaguzi Mkuu mwaka 2017.

Mahakama ya Juu nchini Kenya ina jukumu muhimu la kusikiliza kesi ya kupinga matokeo ya urais nchini humo kama ilivyokuwa mwaka 2013.

Kutokana kutokuwepo kwa Jaji Mkuu, na Majaji wawili katika Mahakama hiyo, ni vigumu sana kwa sasa Mahakama hiyo kuendelea na shughuli zake.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.