Pata taarifa kuu
Rwanda-Ufaransa

Ufaransa yakanusha tuhuma za kuhusika katika mauaji ya kimbari nchini Rwanda

Waziri mkuu mpya wa Ufaransa, Manuel Valls akizungumza kwa mara ya kwanza mbele ya baraza la wawakilishi amesema nchi yake haihusiki na wala haina mkono wowote kwenye mauaji ya kimbari yaliyotokea nchini Rwanda mwaka 1994 na kusababisha mauaji ya wahutu na watutsi laki 8. Matamshi ya waziri mkuu Valls anayatoa wakati huu ambapo kumeibuka mvutano wa maneno kati ya nchi yake na taifa la Rwanda, ambapo hivi karibuni, rais Paul Kagame aliituhumu nchi hiyo kwa kuhusika kwenye machafuko hayo. 

waziri mkuu wa Ufaransa Manuel Vallsakihutubia katika baraza la bunge, April 8, 2014.
waziri mkuu wa Ufaransa Manuel Vallsakihutubia katika baraza la bunge, April 8, 2014. REUTERS/Charles Platiau
Matangazo ya kibiashara

Akizungumza kwa mara ya kwanza tangu kukabidhiwa hatumu ya kuongoza serikali ya Ufaransa, Manuel Valls amesisitza kuwa nchi yake haiwezi kuomba radhi kama inavyodaiwa na serikali ya Rwanda, kwa kuwa haikuwa na jukumu lolote katika mauaji hayo.

Uhusiano kati ya Rwanda na Ufaransa imeendelea kuingia dosari wakati huu Wanyarwanda wakifanya kumbukumbu ya mauaji ya watu wanaokadiriwa kufikia laki nane wa kitutsi pamoja na wahutu wenye msimao wa Wastani.

Waziri wa Sheria Christiane Taubira ambaye angeliwakilisha Ufaransa kwenye sherehe za maadhimisho ya kumbukumbu ya mauaji hayo alilazimika kusitisha ziara yake kufutia kauli ya rais wa Rwanda Paul Kagame ambaye aliituhumu moja kwa moja Ufaransa kuhusika katika mauaji hayo.

Hatuwa hii ilisabisha serikali ya Rwanda kusitisha mualiko na kumzuia balozi wa Rwanda jijini Kigali kushiriki na kuweka shahada la maua katika mnara wa kumbukumbu ya mauaji hayo ya halaiki ya mwaka 1994.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.