Pata taarifa kuu
EBOLA-DRC-JOSEPH KABILA

Juhudi za kunusuru wagonjwa wa Ebola zathitishwa Katika Mji wa beni

Juhudi za kuwasaidia wagonjwa wa Ebola Wilayani Beni Mashariki mwa DRC, na kuhakikisha kuwa hausambai zaidi, zimesitishwa kutokana na makabilano makali kaii ya waasi ya wanajeshi wa Umoja wa Mataifa MONUSCO.

Madakatrai kutoka Shirika la madaktari wasio na mipaka wakikabiliana na ugonjwa wa Ebola nchini DRC
Madakatrai kutoka Shirika la madaktari wasio na mipaka wakikabiliana na ugonjwa wa Ebola nchini DRC ®MSF
Matangazo ya kibiashara

Wizara ya afya nchini humo inasema, mapigano hayo yalizuka siku ya Jumamosi karibu na eneo ambalo watu walioambukizwa Ebola wanakopewa matibabu, lakini pia karibu na hoteli za watalaam wa afya na kuzua wasiwasi.

Jeshi la Umoja wa Mataifa MONUSCO linasema baada ya makabiliano ya saa kadhaa, ilifanikiwa kuwashinda waasi wa ADF Nalu ambao wameendelea kutekeleza mashambulizi na kusababisha juhudi za kupambana na ugonjwa huu kwenda polepole.

Shirika la afya duniani WHO limesema kuwa, wafanyikazi wake 16 walifanikiwa kuokolewa mjini Beni, baada ya kilipuzi kulenga nyumba waliyokuwa wanaishi.

Watalaam wanaonya kuwa iwapo hali hii itaendelea, maambukizi yataendelea kushuhudiwa na idadi ya vifo itaongezeka. Tangu mwezi Agosti, watu 213 wamepoteza maisha.

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.