Pata taarifa kuu
DRC-MAANDAMANO-KABILA

Maandamano dhidi ya rais Kabila kufanyika Jumapili

Waaandamanaji watarejea barabarani kesho katika miji mbalimbali nchini DRC kumshinikiza rais Joseph Kabila kujiuzulu lakini pia kutowania urais mwisho wa mwaka huu.

Maandamano yaliyoandaliwa na Kanisa Katoliki miezi ya hivi karibuni jijini Kinshasa
Maandamano yaliyoandaliwa na Kanisa Katoliki miezi ya hivi karibuni jijini Kinshasa REUTERS/Kenny Katombe
Matangazo ya kibiashara

Maandamano haya yanaratibiwa na Baraza la Maaskofu wa Kanisa Katoliki nchni humo CENCO, ambao wamesema maandamano hayo yataendelea hadi pale matakwa yao yatakapotimizwa.

Maandamano yaliyopita, yalishuhudia makabiliano makali kati ya polisi na waandamanaji na kusababisha zaidi ya watu 10 kupoteza maisha.

Siku ya Ijumaa, kulikuwa na maombi jijini Kinshasa kuombea amani ya DRC kuelekea maandamano hayo ambayo yanatarajiwa kuzua makabiliano makali kati ya waandamanaji na Polisi.

Serikali imekuwa ikizima mtandao ili kuzuia mawasiliano kupitia mitandao ya kijamii pamoja na kutuma ujumbe mfupi wa simu za mkononi, wakati wa maandamano.

Rais Joseph Kabila katika siku zilizopita, amekuwa akilishtumu Kanisa Katoliki kwa kutumia maandamano haya kuwasaidia upinzani kuchukua madaraka kwa nguvu.

Hata hivyo, Maaskofu wa Kanisa hilo lenye ushawishi mkubwa nchini humo wamekanusha madai hayo na kusema, wanashinikiza mabadliko ya kisiasa baada ya kuongoza mchakato wa mazungumzo yalifanikisha mkataba wa kisiasa mwaka 2016.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.