Kusikiliza Pakua Podcast
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 04h30 - 05h00 TU
    Uchambuzi na makala 14/12 04h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 05h30 - 06h00 TU
    Uchambuzi na makala 14/12 05h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 15h00 - 16h00 TU
    Uchambuzi na makala 13/12 15h00 GMT
Ili Kufurahia kikamilifu maudhui ya multimedia yetu, unahitaji kuwa na Plugin iliyowekwa kwenye kompyuta yako Ili kuingia, unahitaji kuruhusu cookies zote kwa kuseti vizuri Ili kutembelea mtandao, tovuti ya RFI inaenda sambamba na Internet Explorer 8 na + Firefox 10 na +, Safari 3 na +, Chrome 17 na + nk
Afrika

DRC: Watu 11 wauawa na wafungwa zaidi ya 900 watoroka kwenye gereza la Beni

media Gereza la Beni, Mashariki mwa DRC RFI Correspodent Reuben Lukumbuka

Watu 11 wamekufa na wafungwa zaidi ya 900 wamefanikiwa kutoroka kwenye gereza moja la mjini Beni mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, mamlaka mjini Goma zimethibitisha.

Akizungumza na idhaa hii, gavana wa jimbo la Goma Julien Paluku amethibitisha kuwa gereza la Kangwayi lililoko mjini Beni lilivamiwa majira ya saa 3 za usiku na watu waliokuwa na silaha na ambao hawajafahamika hadi sasa.

Gavana Paluku amesema kuwa katika majibizano ya risasi na washambuliaji hao watu 11 wamthibitishwa kufa wakiwemo maofisa 8 wa polisi ambapo ameongeza kuwa kati ya wafungwa 966 waliokuwa kwenye gereza hilo ni wafungwa 30 pekee ndio waliobakia.

Gavana huyo ameongeza kuwa mji wa Beni na mji jirani wa Butembo kumetangazwa hali ya dharura ya kutotembea usiku kuanzia saa kumi na mbili na nusu jioni na kwamba ni Polisi na wanajeshi pekee ndio watakaruhusiwa kuonekana muda huo.

Mji huo ulioko kaskazini mwa jimbo linaloshuhudia machafuko la Kivu Kaskazini limeendelea kushuhudia machafuko toka mwaka 2014 ambapo raia zaidi ya 700 wameuawa na wengi kati yao wakiuawa kikatili.

Mauaji haya yamekuwa yakilaumiwa kutekelezwa na waasi wa ADF Nalu, kundi ambalo limekuwa likiundwa na Waislamu wenye msimamo mkali kutoka Uganda ambao awali walikuwa wanataka kuipindua Serikali ya Uganda.

Washukiwa kadhaa pia wa kundi la ADF-Nalu walikuwa wakizuiliwa kwenye gereza la Kangwayi.

Shambulizi kwenye gereza hili limekuja siku moja tu baada ya wapiganaji hao kushambulia kituo cha polisi na ofisi ya mwendesha mashtaka jijini Kinshasa ambapo wameua polisi mmoja na kuwajeruhi wengine kadhaa katika mfululizo wa mashambulizi ya wiki kadhaa.

Tukio hili linajiri pia baada ya matukio mawili ya kuvamiwa kwa magereza nchini humoi katika kipindi cha miezi michache iliyopita ambapo mwezi Mei zaidi ya wafungwa elfu 4 walitoroka kwenye gereza la Kasangulu magharibi mwa Kinshasa pamoja na lile la Makala.

Kuhusu mada hiyo hiyo
 
Samahani, mwunganisho na sava umeshindikana