Pata taarifa kuu
DRC - SIASA

Muungano wa upinzani DRC kumuwekea ngumu mpatanishi, Tshisekedi atarajiwa Lubumbashi

Upinzani nchini Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo chini ya muungano wa vyama vya upinzani vya "Rassemblement", unakataa kushiriki katika hatua ya maandalizi ya "mazungumzo ya kitaifa" inayotarajiwa kuanza siku ya Jumanne chini ya upatanishi wa Umoja wa Afrika (AU) Edem Kodjo.

Etienne Tshisekedi, kiongozi mkuu wa upinzani nchini DRC
Etienne Tshisekedi, kiongozi mkuu wa upinzani nchini DRC AFP PHOTO / JUNIOR DIDI KANNAH
Matangazo ya kibiashara

Katika taarifa iliyosomwa mbele ya waandishi wa habari kwenye makazi ya kiongozi wa upinzani, Etienne Tshisekedi wa Mulumba, muungano huo umebaini kuwa endapo wafungwa wa kisiasa hawataachiwa huru na kesi ambazo ni za kisiasa kufutwa kabisa basi havitashiriki kwenye mazungumzo hayo pamoja na kuwa vipo tayari kushiriki.

Aidha, Muungano huo umeitisha mgomo nchi nzima wiki hii, kupinga kuanzishwa kwa mazungumzo hayo kabla ya masharti yao kutekelezwa, ikiwa ni pamoja na kuwaachia wafungwa wa kisiasa kwa takwimu kuwa kati ya wafungwa 120 walioorodheshwa, ni wafungwa wanne tu ndio walioachiwa huru.

Katika hatua nyingine, juma lijalo, Tshisekedi anatarajiwa jijini Lubumbashi, mji mkuu wa pili kwa ukubwa nchini DRC ambapo atawahutubia wananchi.

Rais wa DRC, Josephu Kabila, ambaye amesema hakuna kitakachozuia kufanyika kwa uchaguzi
Rais wa DRC, Josephu Kabila, ambaye amesema hakuna kitakachozuia kufanyika kwa uchaguzi DR

Ziara hii ataifanya kufuatia ombi la aliyekuwa spika wa bunge jimbo la Katanga, Gabriel Kyungu wa Kumwanza aliyemtembelea hivi karibuni.

Baada ya kuzuru mji wa Lubumbashi Tshisekedi anatarajiwa kuendelea na ziara yake mjini Bukavu au Kindu pamoja na mji wa Goma, ikiwa ni miji ya mashariki mwa jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo ambako usalama umebaki kuwa gumzo na pasua kichwa kwa serikali ya DRC.

Inavyoonekana, Upinzani chini ya Uongozi wa Tshisekedi umeapa kuhakikisha uchaguzi unafanyika ndani ya muda uliopangwa kwa kuzingatia katiba ya nchi ambapo pia utaendelea kuwepo kwa mazingira rafiki ya kufanyika kwa uchagizi wenyewe.

Lakini licha ya yote haya, swali ni kwamba je, Rais Kabila yuko tayari na serikali yake kuwa sikivu wakati huu ambapo hali ya kisiasa nchini humo inaonekana kuwa tete?

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.