Pata taarifa kuu
CHAD-MAANDAMANO-USALAMA

Chad: licha ya kupigwa marufuku, upinzani watoa wito kwa maandamano

Nchini Chad, vyama vya kiraia vimeendelea na msimamo wao wa kuwataka raia kufanya maandamano ya amani yaliopangwa kufanyika Jumanne hii, Aprili 5. Maandamano ambayo yamepigwa marufuku na serikali ya Chad.

Upinzani unapinga Idriss Deby kuwania muhula mwengine katika uchaguzi wa rais wa Aprili 10, nchini Chad.
Upinzani unapinga Idriss Deby kuwania muhula mwengine katika uchaguzi wa rais wa Aprili 10, nchini Chad. © AFP/Issouf Sanogo
Matangazo ya kibiashara

Jumatatu jioni wiki hii, mmoja wa waandaaji wa maandamano hayo, Dc Albissaty Saleh Allazam, aliitishwa polisi na kuwekwa chini ya ulinzi. Anakuwa mtu wa tano wa kutoka vyama vya kiraia kukamatwa.

Muungano wa mashirika na vyama vya wafanyakazi uliojinasibu "Ça suffit" ikimaanisha "Inatosha", ambayo inafanya kazi kwa kumzuia Idriss Deby kugombea kwa awamu ya tano atika uchaguzi wa urais uliopangwa kufanyika Aprili 10, unatarajia kuingia mitaani Jumanne hii Aprili 5 licha ya kupigwa marufuku na Waziri wa Usalama wa umma.

"Tunawafahamisha wananchi kwamba maandamano ya amani kwa ajili ya mabadiliko ya kidemokrasia yatafanyika, Ngandjel Sohhoh Bertrand, msemaji wa "Ça suffit", amesema. Tunasisitiza maandamano yetu ni ya amani. Tunaonya vikosi vya usalama dhidi ya ukandamizaji wowote kwa waandamanaji. "

Waziri wa Usalama wa Umma, ambaye ametoa agizo kwa vikosi vya usalama kuzingira maeneo ambapo kutaonekana kukifanyika mikusanyiko ya hadhara, huku akibaini kwamba kamwe vikosi vya usalam havitofumbia macho jambo hilo.

"Nimechukua uamuzi wa kuzuia maandamano hayo. Licha ya kupigwa marufuku wanataka wakaidi amri hiyo na kuandamana, wajue vizuri kwamba watakuwa katika njia isio halali, Waziri Ahmat Bachir Mahmat, amesema. Na katika mazingira haya watachukuliwa hatua kali. "

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.