Pata taarifa kuu
VATICAN-KANISA-KASHFA YA NGONO

Papa ahimiza maaskofu kusikia kilio cha watoto wadogo wanaomba haki

"Mkutano juu ya ulinzi wa watoto katika Kanisa" imefunguliwa Alhamisi hii, Februari 21 huko Vatican. Mkutano uliosubiriwa na wengi ambao umehudhuria na wakuu wa mabaraza ya maaskofu duniani kote.

Papa Francis amekutana na Wakuu wa Kanisa kutafakari jinsi ya kukabiliana na uhalifu wa makasisi.
Papa Francis amekutana na Wakuu wa Kanisa kutafakari jinsi ya kukabiliana na uhalifu wa makasisi. Vincenzo PINTO / POOL / AFP
Matangazo ya kibiashara

Mkutano huu unalenga kutafutia ufumbuzi halisi wa mgogoro unaokabili Kanisa Katoliki. Mkutano huo umefunguliwa na Papa Francis, ambaye amewataka washiriki kukutaa kwa siku nne mfululizo ili kutafakari aibu hiyo.

Katika hotuba yake ya ufunguzi wa mkutano Papa Francis amesema vitendo vya udhalilishaji wa kingono kwa watoto vitokomezwe na "kuwa fursa ya ufahamu na utakaso".

Papa Francis hajaficha kashfa inayowakabili maaskofu walioalikwa jijini Roma: "Kutokana na kukabiliwa na kashfa ya unyanyasaji wa kijinsia inayofanywa na viongozi wa Kanisa kwa watoto, ninawataka kusikiliza kilio cha watoto ambao wanaomba haki. Watu watakatifu wa Mungu wanatuangalia, na wanatarajia kutoka kwetu si hukumu rahisi na za wazi, lakini hatua halisi na za ufanisi, " amesema Papa Francis

Baada ya utangulizi wa Papa, sauti zilizorekodiwa za ushahidi wa watu watano ambao ni waathirika wa vitendo hivyo zilisikilizwa mbele ya maaskofu wanaoshiriki mkutano huo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.