Kusikiliza Pakua Podcast
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 04h30 - 05h00 TU
    Uchambuzi na makala 19/02 04h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 05h30 - 06h00 TU
    Uchambuzi na makala 19/02 05h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 15h00 - 16h00 TU
    Uchambuzi na makala 18/02 15h00 GMT
Ili Kufurahia kikamilifu maudhui ya multimedia yetu, unahitaji kuwa na Plugin iliyowekwa kwenye kompyuta yako Ili kuingia, unahitaji kuruhusu cookies zote kwa kuseti vizuri Ili kutembelea mtandao, tovuti ya RFI inaenda sambamba na Internet Explorer 8 na + Firefox 10 na +, Safari 3 na +, Chrome 17 na + nk
Utamaduni

Mwanamuziki nguli Charles Aznavour, afariki dunia

media Charles Aznavour wakati akiendesha tamasha, Palais des Sports, Paris Ufaransa, Septemba 2015. RFI / Edmond Sadaka

Mwanamuziki maarufu na muigizaji, raia wa Ufaransa mwenye asili ya Armenia, Charles Aznavour, amefariki dunia usiku wa Jumapili kuamkia Jumatatu wiki hii akiwa na umri wa miaka 94.

Mbali na taaluma yake ya kimataifa katika sanaa, atakumbukwa sana katika harakati zake kwa wananchi wa Armenia kwa kutambua mauaji ya halaiki ya mwaka 1915 na kufanya tarehe hiyo kukumbukwa kila baada ya mwaka. Alikua ni sauti ya wanyonge, raia wa Armenia, ulimwenguni, hasa nchini Ufaransa.

Nchi hii ndogo ya Armenia ina wakazi milioni tatu tu. Lakini raia wake waishio ugenini ni zaidi ya milioni saba. Armenia imemkosa mtu muhimu kwa taifa hilo na wananchi wake, ambaye ni mmoja wa wanaharakati walioweza kuitambulisha Armenia kwa majanga iliyopitia hasa mauaji ya halaki yaliyotokea mwanzoni mwa karne ya ishirini.

Kutoka mwaka 1975, wakati alikuwa tayari kutambuliwa kama nyota wa kimataifa, alitunga moja ya nyimbo zilizopendwa zaidi duniani iliyojulikana kwa jina la: waliangamia. Maneno yaliyomaanisha mauaji ya halaiki ya mwaka 1915 ambayo yalisababisha zaidi ya Waarmenia milioni kuangamizwa.

Mwaka 1988, wakati tetemeko kubwa la ardhi lilipiga katika Jimbo la Spitak kaskazini magharibi mwa Armenia, karibu watu 30,000 walipoteza maisha na zaidi ya 15,000 waliachwa bila makazi. Aznavour, wakati huo aliendesha kampeni ya kuhamasisha misaada kwa watu waliopoteza makaazi yao, aliandika maneno haya Kwako Armenia, wimbo uliotungwa na ndugu yake, Georges Garvarentz, ambaye pia wazazi wake ni raia wa Armenia. Wasanii 24 walijiunga nao. Kupitia wimbo huo, Aznavour alipata umaarufu na ndani na nje ya Armenia.

Miaka kadhaa baadaye, katika mji wa Gyumri, mji ulioathirika na maafa kulijengwa sanamu kwa heshima ya Charles Aznavour.

Mnamo mwaka 2008, akiwa na umri wa 84, mwanamuziki huyo nguli alipewa uraia wa Armenia na aliyekuwa rais wa nchi hiyo Serzh Sargsyan.

Kuhusu mada hiyo hiyo
 
Samahani, mwunganisho na sava umeshindikana