Ushairi ni sanaa inayokua kila kukicha na watunzi wamekua na maana mbalimbali kuhusu ushairi, Senkoro (1988) Katika kitabu chake cha Ushairi, “Nadharia na Tahakiki” anasema ni utanzu wa fasihi utumiao mpangilio wa lugha ya mkato, picha, iliyopangwa kwa njia iletayo mapigo mahususi au yaliyomo ndani yake.Wamitila, (2008) ushairi ni utungo wa sanaa ya lugha na mpangilio maalum wa mishororo, ama kisauti na kwa maneno mateule kwa kubuni mbinu za lugha zenye mnato na mbinu nyingine za kibalagha na kimtindo zinamwezesha mtunzi kuwasilisha ujumbe kwa kifupi na kwa mkokotezo mkubwa unaoelezea hisia, tukio, ama hali kwa lugha ya mvuto.Kwa ujumla ushairi ni sanaa ya lugha ya mkato yenye ughunaji inayosawiri, kueleza au kuonesha jambo, hisia au katika mpangilio mahususi wa maneno wenye urari wa vina na wizani wa sauti.Kutana na Mariagoreth Charles Msanii wa kughani Mashairi kutoka Tanzania akizungumza na Steven Mumbi katika Makala haya.
Vipindi vingine
-
Muziki wa Taarab na chid boy mpiga kinanda wa bendi ya nakshi nakshi
Muziki wa Taarab unashehenezwa na mirindimo ya vyombo kwa kisasa sambamba na Kinanda , Kutana na Chid Boy Mpiga kinanda wa Bendi ya Nakshi Nakshi na Mmiliki wa Bendi hiyo.16/03/202420:07 -
Muziki wa kizazi kipya na Kadason kutoka nchini Tanzania
Sanaa ya muziki wa kizazi kipya.09/03/202420:10 -
Huduma kwa watu wenye ulemavu nchini Tanzania
Hospitali ya Inuka iliyo katika Wilaya ya Makambako Mkoani Njombe nchini Tanzania ni moja ya hospital inayotoa huduma ya utengamao kwa walemavu wa viungo na kuibua tabasamu kwa wana wa taifa hili kutoka mikoa mbali mbali nchini humu.28/02/202409:59 -
Zanzibar: Wasani waliotumbuiza katika tamasha la sauti za busara
Wasani mbali kutoka Afrika walihudhuria tamasha hilo wakiwemo wale wa jamii ya wamaasai kutoka Kenya.24/02/202420:05 -
20:02