Ushairi ni sanaa inayokua kila kukicha na watunzi wamekua na maana mbalimbali kuhusu ushairi, Senkoro (1988) Katika kitabu chake cha Ushairi, “Nadharia na Tahakiki” anasema ni utanzu wa fasihi utumiao mpangilio wa lugha ya mkato, picha, iliyopangwa kwa njia iletayo mapigo mahususi au yaliyomo ndani yake.Wamitila, (2008) ushairi ni utungo wa sanaa ya lugha na mpangilio maalum wa mishororo, ama kisauti na kwa maneno mateule kwa kubuni mbinu za lugha zenye mnato na mbinu nyingine za kibalagha na kimtindo zinamwezesha mtunzi kuwasilisha ujumbe kwa kifupi na kwa mkokotezo mkubwa unaoelezea hisia, tukio, ama hali kwa lugha ya mvuto.Kwa ujumla ushairi ni sanaa ya lugha ya mkato yenye ughunaji inayosawiri, kueleza au kuonesha jambo, hisia au katika mpangilio mahususi wa maneno wenye urari wa vina na wizani wa sauti.Kutana na Mariagoreth Charles Msanii wa kughani Mashairi kutoka Tanzania akizungumza na Steven Mumbi katika Makala haya.
Vipindi vingine
-
Zanzibar: Fahamu zaidi kuhusu Muziki wa Baibuda katika makala haya
Mwandishi wetu Steven Mumbi amezungumza na msani wa muziki huu wa Baibuda13/04/202420:09 -
Afrobongo na Bruce Africa
Makala haya hukuletea historia ya sanaa na wasani barani Afrika.06/04/202420:03 -
Sanaa ya muziki wa kizazi kipya na Sam Silver
Sam Silver anazungumza naye Steve Mumbi katika makala ya Nyumba ya Sanaa wiki hii.30/03/202420:03 -
Muziki wa Taarab na chid boy mpiga kinanda wa bendi ya nakshi nakshi
Muziki wa Taarab unashehenezwa na mirindimo ya vyombo kwa kisasa sambamba na Kinanda , Kutana na Chid Boy Mpiga kinanda wa Bendi ya Nakshi Nakshi na Mmiliki wa Bendi hiyo.16/03/202420:07 -
Muziki wa kizazi kipya na Kadason kutoka nchini Tanzania
Sanaa ya muziki wa kizazi kipya.09/03/202420:10