Pata taarifa kuu
Nyumba ya Sanaa

Mariagoreth:Ushairi una nafasi ya kuleta Mabadiliko

Imechapishwa:

Ushairi ni sanaa inayokua kila kukicha na watunzi wamekua na maana mbalimbali kuhusu ushairi, Senkoro (1988) Katika kitabu chake cha Ushairi, “Nadharia na Tahakiki” anasema ni utanzu wa fasihi utumiao mpangilio wa lugha ya mkato, picha, iliyopangwa kwa njia iletayo mapigo mahususi au yaliyomo ndani yake.Wamitila, (2008) ushairi ni utungo wa sanaa ya lugha na mpangilio maalum wa mishororo, ama kisauti na kwa maneno mateule kwa kubuni mbinu za lugha zenye mnato na mbinu nyingine za kibalagha na kimtindo zinamwezesha mtunzi kuwasilisha ujumbe kwa kifupi na kwa mkokotezo mkubwa unaoelezea hisia, tukio, ama hali kwa lugha ya mvuto.Kwa ujumla ushairi ni sanaa ya lugha ya mkato yenye ughunaji inayosawiri, kueleza au kuonesha jambo, hisia au katika mpangilio mahususi wa maneno wenye urari wa vina na wizani wa sauti.Kutana na Mariagoreth Charles Msanii wa kughani Mashairi kutoka Tanzania akizungumza na Steven Mumbi katika Makala haya.

Mariagoreth Charles Msanii wa Kughani Mashairi kutoka nchini Tanzania
Mariagoreth Charles Msanii wa Kughani Mashairi kutoka nchini Tanzania Mariagoreth/Poetry
Vipindi vingine
  • 20:07
  • 20:10
  • 09:59
  • 20:05
  • 20:02
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.