Pata taarifa kuu
AFRIKA KUSINI-SANAA

Mwanamuziki maarufu wa mtindo wa jazz kutoka Afrika Kusini afariki dunia

Afrika Kusini imepoteza mwanamuziki maarufu wa mtindo wa jazz Hugh Masekela, ambaye alikua mmoja wa wanaharakati dhidi ya ubaguzi wa rangi nchini huo.

Hugh Masekela katika tamasha Paris mnamo mwaka  2010.
Hugh Masekela katika tamasha Paris mnamo mwaka 2010. RFI / Edmond Sadaka
Matangazo ya kibiashara

Hugh Masekela alifariki leo Jumanne akiwa na umri wa miaka 78, na hivyo kuzua hisia mbalimbali, huku watu wengi wakikaribisha ujumbe uliomo katika nyimbo zake na dhamira yake ya kisiasa.

"Ni kwa huzuni mkubwa familia ya Ramapolo Hugh Masekela inatangaza kifo chake. Baada ya vita jasiri dhidi ya saratani ya kibofu, Hugh Masekela amefariki katika mji wa Johannesburg, akizungukwa na familia yake, "familia yake ilisema. Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma amekaribisha ujasiri wa "mwanamuziki huyo wa mtindo wa jazz, mcheza tarumbeta, mlinzi wa utamaduni na mkongwe wa harakati za ukombozi" dhidi ya ubaguzi wa rangi. "Aliendelea kutetea uhuru kupitia nyimbo zake dhidi ya ubaguzi wa rangi, " Zuma amesema. "Ulimwengu wa wanamuziki hasa Afrika kusini umepoteza nguzo kubwa. "

Alikabiliwa na umaskini, ubaguzi na kulazimika kutorka nchi, lakini pia umaarufu na kufanya ziara katika nchi mbalimbali duniani.

Masekela alipata umaarufu mkubwa kutokana na mtindo wake wa kipekee wa Afro-Jazz na vibao vilivyokuwa maarufu kama vile Soweto Blues. Wimbo ambao alioutoa 1977 na ulihusi

Akiwa na umri wa miaka 14 alianza kupiga tarumbeta baada ya kutizama filamu ya hollywood kumhusu mwanamuziki wa Kimarekani mwa mtindo wa Jazz.ka sana katika harakati za kupambana na utawala wa ubaguzi wa rangi nchini Afrika kusini.

Masekela alipata umaarufu mkubwa kutokana na mtindo wake wa kipekee wa Afro-Jazz na vibao vilivyokuwa maarufu kama vile Soweto Blues.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.