Pata taarifa kuu
UFARANSA-SANAA

Mwanamuziki nguli Johnny Hallyday afariki dunia

Johnny Hallyday, mwanamuziki nguli wa mitindo ya Rock-star amefariki dunia usiku wa Jumanne Desemba 6 kuamkia Jumatano Desemba 6 akiwa na umri wa miaka 74, kufuatia saratani ya mapafu, mkewe Laeticia ameliambia shirika la habari la AFP.

Johnny Hallyday, katika mji wa Villeneuve d'Ascq, Julai 2003.
Johnny Hallyday, katika mji wa Villeneuve d'Ascq, Julai 2003. Photorock/Frédéric Loridant
Matangazo ya kibiashara

Johnny Hallyday alikua mwanamuziki wa kuigwa. Kwa zaidi ya miaka hamsini, Ufaransa ilijikita sana na nyimbo zake lakini pia upendo wake, pikipiki zake, watoto wake, safari zake na katuni zake.

Johnny ni rafiki wa vizazi kadhaa vya Ufaransa katika enzi hizo. Johnny Hallyday alicheza nyimbo nyingi. Nyimbo zake zilipendwa na zinaendelea kupendwa na mamilioni ya watu duniani, hasa nchini Ufaransa.

Ubunifu wa Johnny uligusa jamii zote nchini Ufaransa. Tangu asubuhi katika miaka ya 1960, hakuna Mfaransa aliyeishi bila kukutana na Johnny au kusikiliza nyimbo zake.

"Kuna Johnny wa kila mtu na Johnny wa watu wote, Johnny anayekasirisha na Johnny anaefurahisha, kuna Johnny ambaye anastahiliwa na Johnny amesamehewa kwa kila kitu, " baadhi ya wakazi wa Paris wameeleza.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.