Kusikiliza Pakua Podcast
 • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 04h30 - 05h00 TU
  Uchambuzi na makala 18/02 04h30 GMT
 • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 05h30 - 06h00 TU
  Uchambuzi na makala 18/02 05h30 GMT
 • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 15h00 - 16h00 TU
  Uchambuzi na makala 17/02 15h00 GMT
Ili Kufurahia kikamilifu maudhui ya multimedia yetu, unahitaji kuwa na Plugin iliyowekwa kwenye kompyuta yako Ili kuingia, unahitaji kuruhusu cookies zote kwa kuseti vizuri Ili kutembelea mtandao, tovuti ya RFI inaenda sambamba na Internet Explorer 8 na + Firefox 10 na +, Safari 3 na +, Chrome 17 na + nk
Habari mpya kabisa
 • Uingereza: Wabunge saba watangaza kujiuzulu kwa sababu ya Brexit na ubaguzi wa rangi
 • Askari wanne wa India wauawa kwa kupigwa risasi Kashmir (polisi)
 • Paris yaona kuwa "hakuna sababu" ya kupinga kusafirishwa kwa "magaidi" ambao Italia inaomba (waziri)
 • Poland haitoshiriki mkutano wa kundi la Visegrad nchini Israeli
 • Berlin yaona kuwa "ni vigumu" wanajihadi kutoka Ulaya kurejea nyumbani
Utamaduni

Agizo la kudhibiti matumizi ya ngoma ya utamaduni lazua utata Burundi

media Wapiga ngoma ya utamaduni wa Burundi. MARCO LONGARI / AFP

Rais wa Burundi Pierre Nkurunziza, amepiga marufuku wanawake kushiriki katika ngoma za kiutamaduni katika shughuli za kiserikali zinazofanyika nchini humo.

Hatua hiyo inakuja ukiwa ni mpango wa kudhibiti vikundi vya kutumbuiza kwa kutumia ngoma za asili pamoja na kupiga marufuku watoto wa kike kushiriki katika ngoma hizo.

Hatua hii imekosolewa na baadhi ya wakazi wa mji wa Bujumbura ambao wengi wao wamekua wakitumia ngoma hii kwa sherehe za harusi. Lakini wakazi wengine wamekaribish ahatua hii wakisema ngoma ya utamaduni ya Burundi imekua imepotza thamani kutokana na kutumiwa hovyo kwa sherehe zisizo kuwa na manufaa kwa tailfa hilo.

"Zaidi ya kuwa ishara kamili ya ufalme nchini Burundi, vijiti na mchezo wa ngoma hiyo pia vinawakilisha msimamo wa kiume, na ngoma inawakilisha mwili wa mwanamke. Kwa hivyo marufuku iliyotolewa dhidi ya wanawake kugusa au kukaribia ngome hiyo ni sahihi", amesema mmoja wa wapiga ngoma ya utamaduni. Hadithi ambayo imebaki hai katika Burundi ya kisasa.

Lakini shirika moja la haki za binadamu nchini humo linasema kuwa agizo hilo linatakiwa lifutwe, kwa sababu linakiuka katiba ya nchi. "Agizo hili linakiuka ibara ya 22 ya Katiba ya Burundi ambayo inasema kuwa hakuna Mrundi wowote ule ambaye anaweza kubaguliwa kwa aina yoyote, sawa na jinsia yake, dini yake, kabila au chama chake cha siasa", amesea kiongozi wa Fenadeb, Jacques Nshimirimana.

Kwa upande wake Pacific Nininahazwe, mmoja wa viongozi wa mashirika ya vyama vya kiraia aliye uhamishoni, anaamini kwamba "kwa agizo hili, raia wa Burundi hana tena haki kwa ngoma ya utamaduni, ila kwa serikali pekee".

Shirika la umoja wa mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni, UNESCO, mwaka 2014 liliorodhesha Ngoma ya kiutamaduni ya kifalme nchini Burundi katika Urithi wa Kitamaduni wa dunia.

Kuhusu mada hiyo hiyo
 
Samahani, mwunganisho na sava umeshindikana