Pata taarifa kuu
BURUNDI-UTAMADUNI-NGOMA

Agizo la kudhibiti matumizi ya ngoma ya utamaduni lazua utata Burundi

Rais wa Burundi Pierre Nkurunziza, amepiga marufuku wanawake kushiriki katika ngoma za kiutamaduni katika shughuli za kiserikali zinazofanyika nchini humo.

Wapiga ngoma ya utamaduni wa Burundi.
Wapiga ngoma ya utamaduni wa Burundi. MARCO LONGARI / AFP
Matangazo ya kibiashara

Hatua hiyo inakuja ukiwa ni mpango wa kudhibiti vikundi vya kutumbuiza kwa kutumia ngoma za asili pamoja na kupiga marufuku watoto wa kike kushiriki katika ngoma hizo.

Hatua hii imekosolewa na baadhi ya wakazi wa mji wa Bujumbura ambao wengi wao wamekua wakitumia ngoma hii kwa sherehe za harusi. Lakini wakazi wengine wamekaribish ahatua hii wakisema ngoma ya utamaduni ya Burundi imekua imepotza thamani kutokana na kutumiwa hovyo kwa sherehe zisizo kuwa na manufaa kwa tailfa hilo.

"Zaidi ya kuwa ishara kamili ya ufalme nchini Burundi, vijiti na mchezo wa ngoma hiyo pia vinawakilisha msimamo wa kiume, na ngoma inawakilisha mwili wa mwanamke. Kwa hivyo marufuku iliyotolewa dhidi ya wanawake kugusa au kukaribia ngome hiyo ni sahihi", amesema mmoja wa wapiga ngoma ya utamaduni. Hadithi ambayo imebaki hai katika Burundi ya kisasa.

Lakini shirika moja la haki za binadamu nchini humo linasema kuwa agizo hilo linatakiwa lifutwe, kwa sababu linakiuka katiba ya nchi. "Agizo hili linakiuka ibara ya 22 ya Katiba ya Burundi ambayo inasema kuwa hakuna Mrundi wowote ule ambaye anaweza kubaguliwa kwa aina yoyote, sawa na jinsia yake, dini yake, kabila au chama chake cha siasa", amesea kiongozi wa Fenadeb, Jacques Nshimirimana.

Kwa upande wake Pacific Nininahazwe, mmoja wa viongozi wa mashirika ya vyama vya kiraia aliye uhamishoni, anaamini kwamba "kwa agizo hili, raia wa Burundi hana tena haki kwa ngoma ya utamaduni, ila kwa serikali pekee".

Shirika la umoja wa mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni, UNESCO, mwaka 2014 liliorodhesha Ngoma ya kiutamaduni ya kifalme nchini Burundi katika Urithi wa Kitamaduni wa dunia.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.