Harusi za usiku zapigwa marufuku Mombasa
Sasa ni ni marufuku kuandaa sherehe za harusi usiku katika mji wa Mombasa, kusini mwa Kenya. Mkuu wa polisi katika kaunti ya Mombasa, Maalim Mohammed ameeleza kwamba hatua hii ina lengo la kuimarisha usalama katika eneo hilo.
Imechapishwa:
Kwa hauta hii wakazi wa mji watalindwa kutokana na mashambulizi ya visu na yanayoendeshwa na magenge ya watu.
Hivi karibuni, makundi ya uhalifu yameongezeka mjini Mombasa.
Katika baadhi ya vitongoji, watu wana wamearifu kuwa vitendo vya ujambazi vimekua vikifanyika mchana kweupe.
Wahalifu wengi kutoka makundi hayo tayari wamekamatwa na polisi ambayo inaendelea na shughuli hizokatika maeneo mbalimbali.
Kwa ujumla, sherehe za harusi zinadumu hadi siku tano mjini Mombasa, pamoja na sikukuu siku nzima na usiku.