Pata taarifa kuu
UFARANSA-DINI-UGAIDI

Ufaransa: Burkini yapigwa marufuku

Nguo hiii ya kuogea, inayovaliwa na baadhi ya wanawake wa Kiislamu, inayofunika mwili mzima isipokuwa uso, miguu na mikono, imezua utata. Miji minne nchini Ufaransa imeamua kupiga marufuku vazi hili kwenye fukwe zao.

Burkini aina ya Marks na Spencer.
Burkini aina ya Marks na Spencer. DR.
Matangazo ya kibiashara

Viongozi tawala katika mkoa wa Touquet (Pas-de-Calais) wameamua Jumanne hii Agosti 16 kukataza kwa upande wao kuvaa Burkini ili "kupiga vita masuala ya kidini," anasema Mkuu wa mkoa huo kutoka chama cha Republican, Daniel Fasquelle. "Hakuna kuvaa Burkini kwa sasa katika mkoa wa Touquet, lakini sitaki idara zangu zichukulie suala hili kama muhimu kama vile utadhani tumeathirika na jambo hili," ameonya Mkuu wa mkoa wa Touquet. Amri yake itaanza kutekelezwa mnamo wiki.

Katika mji wa Corsica, Burkini imezua vurugu

Jumatatu hii, mji mdogo wa Sisco (katika eneo la Haute-Corse), watu 1000, walipiga marufuku nguo hii kwenye fukwe. Mkuu wa mji, Ange-Pierre Vironi, kutok chama cha PS alichukua uamuzi kufuatia rabsha iliyotokea Jumamosi. Familia ya watu wenye ya Afrika Kaskazini na watu kutoka jamii ya Corse walirushiana mawe na wengine kuchomana visu, hali ambayo ilisababisha watu watano kujeruhiwa. Akari polisi zaidi ya mia moja walitumwa katika eneo hilo ili kurejesha utulivu.

Uchunguzi umeanzishwa, lakini kuoga na Burkini ni sababu ya vurugu. Mashahidi wanasema kwamba familia ya watu wenye asili ya Afrika Kaskazini hawakufurahishwa kuona kwamba wanawake wa kundi lao, ambao walikua wakioga wakijifunika mwili mzima, waweze kupigwa picha.

Mwishoni mwa mwezi Julai, Mkuu wa mji wa Cannes, kusini mwa Ufaransa, alikuwa wa kwanza kupiga marufuku uvaaji wa Burkini. David Lisnard (Republican) alijitetea akitoa sababu ya haja ya kuvaa ufukweni nguo za kawaida "mavazi sahihi, ya heshima kimaadili na yasiyokuwa na misimamo ya dini yoyote".

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.