Kusikiliza Pakua Podcast
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 04h30 - 05h00 TU
    Uchambuzi na makala 18/09 04h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 05h30 - 06h00 TU
    Uchambuzi na makala 18/09 05h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 15h00 - 16h00 TU
    Uchambuzi na makala 18/09 15h00 GMT
Ili Kufurahia kikamilifu maudhui ya multimedia yetu, unahitaji kuwa na Plugin iliyowekwa kwenye kompyuta yako Ili kuingia, unahitaji kuruhusu cookies zote kwa kuseti vizuri Ili kutembelea mtandao, tovuti ya RFI inaenda sambamba na Internet Explorer 8 na + Firefox 10 na +, Safari 3 na +, Chrome 17 na + nk
Utamaduni

DRC: Koffi Olomide asalia jela

media Mwanamuziki maarufu wa DRC, Koffi Olomide mbele ya mahakama mjini Kinshasa tarehe 16 Agosti 2012. (Picha ya zamani) JUNIOR KHANNA / AFP

Koffi Olomide hatimaye amewekwa kizuizini. Wanasheria wake hawakuweza kupata dhamana kwa nyota huyo wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, ambaye ameshitakiwa kumpiga mmoja wa wachezaji wake nchini Kenya.

Tukio hili lilirekodiwa na limesambazwa kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii. Msanii huyu maarufu wa Congo atasalia jela kwa siku zaidi ya kumi na tano. Uamuzi ambo umepingwa na mwanasheria wake Ruffin Lukoo.

Koffi Olomide, alikamatwa jijini Kinshasa kwa kosa la kumpiga teke mnenguaji wake wa kike jijini Nairobi nchini Kenya mwishoni mwa juma lililopita.

Masaibu ya Olomide yameendelea kushuhudiwa kwa juma la pili baada ya kukamatwa na kufukuzwa nchini Kenya kutokana na tukio hilo, na tamasha lake kusitishwa.

Polisi nchini DRC wanasema mwanamuziki huyo mwenye umri wa miaka 60 anashikiliwa kwa mahojiano zaidi kutokana na tukio la Nairobi.

Jumapili iliyopita, Olomide alihojiwa na Televisheni moja nchini humo akiomba msamaha kwa kitendo alichofanya.

"Hii sio mara ya kwanza kwa mwanamuziki huyu kujipata katika hali hii", wamesema baadhi yawanenguaji wake waliotengana naye baada ya visa kama hivyo, na kuamua kujiunga bendi nyingine nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

Kuhusu mada hiyo hiyo
 
Samahani, mwunganisho na sava umeshindikana