Pata taarifa kuu
EAC-UTAMADUNI

Mkutano kuhusu Historia na vitabu Afrika wafanyika Dar es Salaam

Raia wa Afrika Mashariki wametakiwa kujenga utamaduni wa kusoma, kufanya tafiti na kuandika vitabu vya historia yao ili kuchota maarifa mbalimbali na kuwasaidia katika kufanya shughuli za maendeleo na kutunza Histori yao.

Wanafunzi wa shule ya sekondari Kabanga Ngara Tanzania.
Wanafunzi wa shule ya sekondari Kabanga Ngara Tanzania. Julian Rubavu / RFI
Matangazo ya kibiashara

Wito huo ulitolewa na mchapishaji mkongwe wa vitabu, hususan vitabu vya Kiswahili Walter Bgoya wakati wa mdahalo kuhusu uandishi wa vitabu vya kihistoria uliofanyika jijini dar es salaam

Kushindwa kwa Wanazuoni wengi wa Kiafrika kuandika historia yao Kumechangia katika upotoshwaji mkubwa wa hitoria ya Waafrika.

Chambi Chachage mwanafunzi wa shada ya uzamili ya Historia katika chuo kikuu cha Harvad nchini Marekani,amewataka raia wa Afrika Mashariki kutekeleza wito huo wa kujenga utamaduni wa kusoma, kufanya tafiti na kuandika vitabu vya historia yao.

Huu ni miongoni mwa midahalo ambayo imekuwa ikiandaliwa na Ubalozi wa Ufaransa nchini Tanzania kwa ushirikiano na wadau mbalimbali, kuimarisha uhusiano wa nchi hizo mbili.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.