Kusikiliza Pakua Podcast
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 04h30 - 05h00 TU
    Uchambuzi na makala 19/02 04h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 05h30 - 06h00 TU
    Uchambuzi na makala 19/02 05h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 15h00 - 16h00 TU
    Uchambuzi na makala 18/02 15h00 GMT
Ili Kufurahia kikamilifu maudhui ya multimedia yetu, unahitaji kuwa na Plugin iliyowekwa kwenye kompyuta yako Ili kuingia, unahitaji kuruhusu cookies zote kwa kuseti vizuri Ili kutembelea mtandao, tovuti ya RFI inaenda sambamba na Internet Explorer 8 na + Firefox 10 na +, Safari 3 na +, Chrome 17 na + nk
Utamaduni

Watu karibu ya 100 wauwawa katika machafuko mjini Abyei

media Mji wa Abyei, eneo lililo na utajiri wa mafuta, katika mpaka wa Sudan Kaskazini na Kusini. (Photo: Reuters)

Watu wanaokadiriwa kufikia mia moja wameuawa nchini Sudan, katika eneo lenye utajiri wa mafuta la Abyei, wakati Majeshi ya Sudan Kaskazini yalipovamia eneo hilo na kuchangia kuzuka kwa machafuko.
Takwimu hizo zimetolewa na Deng Arop Kuol, aliyekuwa Kiongozi wa Abyei kabla ya kutimuliwa kwenye wadhifa wake na Rais wa nchi hiyo Omar Hassan Al-Bashir. Kuol, ameongeza kuwa hali imezidi kuwa mbaya huku wananchi wakihitaji misaada zaidi ya kibinadamu.

Kwa upande wa Vikosi vya Umoja wa Mataifa (UN) vinavyoshika doria nchini Sudan kupitia Msemaji wao Hua Jiang, amesema wameendelea kushuhudia maiti mitaani wakati wakiwa kwenye doria zao.

Abyei, ni eneo ambalo, kutokana na utajiri wake wa mafuta- rasilimali muhimu kwa ukuaji wa taifa hilo, limeshuhudia mapigano makali baina ya majeshi ya Kaskazini na Kusini, ambayo kila mmoja inagombania eneo hilo, liwe mali yake.

Kufuatia kadhia hiyo, iliyodumu kwa miaka mingi, hatimaye raia wa Sudan Kusini walipata fursa ya kupiga kura ya maamuzi mnamo tarehe 9 Januari, mwaka huu.

Zoezi hilo lilifanikisha ndoto ya raia wengi wa Sudan Kusini, ambao walisherehekea maamuzi hayo usiku na mchana.

 

 

 
Samahani, mwunganisho na sava umeshindikana